Yunus 10:81
يونسفَلَمَّآ أَلْقَوْا۟ قَالَ مُوسَىٰ مَا جِئْتُم بِهِ ٱلسِّحْرُ ۖ إِنَّ ٱللَّهَ سَيُبْطِلُهُۥٓ ۖ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يُصْلِحُ عَمَلَ ٱلْمُفْسِدِينَ
Basi walipotupa, Musa akasema: Mliyoleta ndiyo uchawi. Hakika Mwenyezi Mungu ataubatilisha. Hakika Mwenyezi Mungu hayatengenezi matendo ya waharibifu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Walipo tupa, Musa alisema: Mliyo leta ni uchawi. Hakika Mwenyezi Mungu haitengenezi kazi ya waharibifu. [81]
[81] Walipo tupa kamba zao na fimbo zao, Musa aliwaambia: Huo mlio fanya ni uchawi kweli, na Mwenyezi Mungu Subhanahu atauvunja kwa mkono wangu! Hakika Mwenyezi Mungu hawasahilishii mafisadi vitendo vyao vikawa vizuri na vyenye nafuu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Walipozitupa kamba zao na fimbo zao, Mûsã aliwaambia, «Mlivyokuja navyo mkavitupa ni uchawi. Allah Mtukufu Ataviondoa mlivyokuja navyo na atavitengua. Hakika Allah Mtukufu Hakitengenezi kitendo cha anayetembea katika ardhi ya Allah Mtukufu kufanya mambo Anayoyachukia na kufanya uharibifu humo kwa kumuasi».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net