Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 10 · Aya ya 78

Yunus 10:78

يونس

قَالُوٓا۟ أَجِئْتَنَا لِتَلْفِتَنَا عَمَّا وَجَدْنَا عَلَيْهِ ءَابَآءَنَا وَتَكُونَ لَكُمَا ٱلْكِبْرِيَآءُ فِى ٱلْأَرْضِ وَمَا نَحْنُ لَكُمَا بِمُؤْمِنِينَ

Maana

Wakasema: Je, umetujia ili utuachishe tuliyowakuta nayo baba zetu, na mpate nyinyi wawili ukubwa katika ardhi? Wala sisi hatuwaamini nyinyi.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wakasema: Je! Umetujia ili utuachishe tuliyo wakuta nayo baba zetu, na mpate nyinyi wawili ukubwa katika nchi? Wala sisi hatukuaminini nyinyi. [78]

[78] Firauni na watu wake walimwambia Musa: Hapana shaka wewe umekuja kwa makusudi ya kutuachisha dini ya baba zetu, na mila za kaumu yetu, ili nyinyi wawili mpate kuwa na wafuasi; wewe na nduguyo mpate ufalme na utukufu na urais wa kutawala na kuhukumu! Kwa hivyo basi sisi hatutakuaminini nyinyi wala huo utume wenu!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Fir‛awn na kundi lake wakasema kumwambia Mûsã, «Je, umetujia kutuepusha na yale ambayo tuliwakuta nayo wazazi wetu ya kuabudu asiyekuwa Allah Mtukufu, mupate kuwa na utukufu na mamlaka, wewe na Hãrûn, katika ardhi ya Misri? Basi sisi si wenye kukubali kwamba wawili nyinyi ni Mitume mliotumwa kwetu ili tumuabudu Allah Mtukufu, Peke Yake, Asiye na mshirika».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yunus

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net