Yunus 10:79
يونسوَقَالَ فِرْعَوْنُ ٱئْتُونِى بِكُلِّ سَـٰحِرٍ عَلِيمٍ
Na Firauni akasema: Nileteeni kila mchawi ajuaye zaidi!
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na Firauni akasema: Nileteeni kila mchawi mjuzi! [79]
[79] Firauni na kaumu yake wakadai kuwa Musa na nduguye ni wachawi, wala si Mitume! Akawataka watu wake wamhudhurishe kila aliye hodari katika fani za uchawi katika mamlaka yake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na akasema Fir‛awn, «Nileteeni kila mchawi mwenye uhodari wa uchawi».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net