Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 10 · Aya ya 77

Yunus 10:77

يونس

قَالَ مُوسَىٰٓ أَتَقُولُونَ لِلْحَقِّ لَمَّا جَآءَكُمْ ۖ أَسِحْرٌ هَـٰذَا وَلَا يُفْلِحُ ٱلسَّـٰحِرُونَ

Maana

Akasema Musa, "Je, mnasema hivi juu ya haki ilipowajia? Je, huu ni uchawi? Na wachawi hawafanikiwi!"

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Akasema Musa: Mnasema hivi juu ya Haki ilipo kujieni? Huu ni uchawi? Na wachawi hawafanikiwi! [77]

[77] Musa akawaambia kukanya uzushi wao: Nyinyi mnaita Haki iliyo toka kwa Mwenyezi Mungu kuwa ni uchawi? Hivyo hii kweli mliyo iona kwa macho yenu ni uchawi? Basi hivi hapa mimi nakutakeni mthibitishe kwamba huu ni uchawi. Waleteni wachawi wathibitishe hayo mnayo yadai. Na wachawi hawafanikiwi abadan!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Mûsã aliwaambia akiona ajabu kwa maneno yao, «mnaiambia haki ilipowajia kuwa ni uchawi? Tazameni sifa za kitu kilichowajia na vilivyomo ndani yake, mtakikuta ni ukweli. Na wachawi hawafaulu wala hawafuzu ulimwenguni wala Akhera».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yunus

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net