Yunus 10:63
يونسٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَكَانُوا۟ يَتَّقُونَ
Wale walioamini na wakawa wachaji.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hao ni ambao wameamini na wakawa wanamcha Mungu. [63]
[63] Na hao ndio walio yasadiki yote yaliyo toka kwa Mwenyezi Mungu, na wakaifuata Haki, na wakayaepuka maasi, na wakamkhofu Mwenyezi Mungu katika kila walitendalo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Sifa za Mawalii hawa ni kwamba wao wamemuamini Allah Mtukufu na wamemfuata Mtume Wake na yale ambayo alikuja nayo kutoka kwa Allah Mtukufu na kwamba wao wanamcha Allah Mtukufu kwa kuzifuata amri Zake na kuyaepuka matendo ya kumuasi.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net