Yunus 10:62
يونسأَلَآ إِنَّ أَوْلِيَآءَ ٱللَّهِ لَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ
Jueni kuwa vipenzi wa Mwenyezi Mungu hawana hofu yoyote juu yao wala hawatahuzunika.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Jueni kuwa vipenzi vya Mwenyezi Mungu hawatakuwa na khofu wala hawatahuzunika. [62]
[62] Enyi watu! Tanabahini na mjue ya kuwa wenye kumuelekea Mwenyezi Mungu kwa Imani na ut'iifu Yeye anawapenda, na wao wanampenda. Hawana khofu ya kuhizika duniani, wala kupata adhabu ya Akhera. Wala wao hawahuzuniki kwa kukosa starehe za duniani, kwa kuwa watapata kwa Mwenyezi Mungu yaliyo makubwa na mengi kuliko hayo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Jueni mtanabahi kwamba mawalii wa Allah Mtukufu hawatakuwa na woga wa mateso ya Allah Mtukufu Akhera, wala wao hawatasikitika juu ya hadhi za kilimwengu walizozikosa.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net