Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 10 · Aya ya 61

Yunus 10:61

يونس

وَمَا تَكُونُ فِى شَأْنٍ وَمَا تَتْلُوا۟ مِنْهُ مِن قُرْءَانٍ وَلَا تَعْمَلُونَ مِنْ عَمَلٍ إِلَّا كُنَّا عَلَيْكُمْ شُهُودًا إِذْ تُفِيضُونَ فِيهِ ۚ وَمَا يَعْزُبُ عَن رَّبِّكَ مِن مِّثْقَالِ ذَرَّةٍ فِى ٱلْأَرْضِ وَلَا فِى ٱلسَّمَآءِ وَلَآ أَصْغَرَ مِن ذَٰلِكَ وَلَآ أَكْبَرَ إِلَّا فِى كِتَـٰبٍ مُّبِينٍ

Maana

Na huwi katika jambo lolote, wala husomi sehemu yoyote katika Qur-ani, wala hamtendi kitendo chochote isipokuwa Sisi huwa ni mashahidi juu yenu mnaposhughulika nayo. Na hakifichikani kwa Mola wako Mlezi chenye uzito hata wa chembe katika ardhi na katika mbingu, wala kidogo kuliko hicho wala kikubwa isipokuwa kimo katika Kitabu kibainifu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na huwi katika jambo lolote, wala husomi sehemu yoyote katika Qur'ani, wala hamtendi kitendo chochote ila Sisi huwa ni mashahidi juu yenu mnapo shughulika nayo. Na hakifichikani kwa Mola wako Mlezi chenye uzito hata wa chembe katika ardhi na katika mbingu, wala kidogo kuliko hicho wala kikubwa ila kimo katika Kitabu kilicho wazi. [61]

[61] Ewe Mtume! Hakika wewe umefikisha ujumbe wako, na hayo Mwenyezi Mungu anayajua. Na hapana jambo lolote katika mambo yako, na huwasomei Qur'ani, na wewe na umma wako hamtendi kitu, ila Sisi tunayashuhudia na tunayaangalia mnapo yaingia kwa juhudi. Na Mola wako Mlezi haachi kujua chochote hata kikiwa kina uzito wa chembe hichi, ikiwa katika mbingu au katika ardhi, kidogo na kikubwa. Vyote hivyo vinadhibitiwa katika Kitabu kilichoko kwa Mwenyezi Mungu, nacho ni chenye kubainisha wazi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na huwi, ewe Mtume, kwenye jambo lolote katika mambo yako, na husomi chochote kile katika aya za Kitabu cha Allah Mtukufu, na hafanyi yoyote katika ummah huu tendo lolote lema au baya, isipokuwa sisi huwa ni mashahidi juu yenu ni wenye kuliona hilo, mnapolichukua na kulitenda, tukawahifadhia na tukawalipa kwalo. Na haufichamani na ujuzi wa Allah Mtukufu uzito wa chungu mdogo ardhini wala mbinguni, wala kitu kidogo kabisa wala kikubwa kabisa, isipokuwa kiko kwenye Kitabu kilichoko kwa Allah Mtukufu kilicho waziwazi chenye ufafanuzi, ujuzi Wake umekizunguka na Kalamu Yake imekiandika.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yunus

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net