Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 10 · Aya ya 60

Yunus 10:60

يونس

وَمَا ظَنُّ ٱلَّذِينَ يَفْتَرُونَ عَلَى ٱللَّهِ ٱلْكَذِبَ يَوْمَ ٱلْقِيَـٰمَةِ ۗ إِنَّ ٱللَّهَ لَذُو فَضْلٍ عَلَى ٱلنَّاسِ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَشْكُرُونَ

Maana

Na ni nini dhana ya wale wanaomzulia Mwenyezi Mungu uongo Siku ya Kiyama? Hakika Mwenyezi Mungu ni mwenye fadhila juu ya watu, lakini wengi wao hawashukuru.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na nini dhana ya wanao mzulia Mwenyezi Mungu kwa Siku ya Kiyama? Hakika Mwenyezi Mungu ana fadhila juu ya watu, lakini wengi wao hawashukuru. [60]

[60] Na watadhani nini Siku ya Kiyama hao walio mzulia uwongo Mwenyezi Mungu, wakajipa kuhalalisha na kuharimisha bila ya kuwa nayo dalili yoyote? Hakika Mwenyezi Mungu amewaneemesha neema nyingi na amezihalalisha kwao kwa fadhila yake, na amewawekea Sharia yenye kheri kwao. Lakini hawamshukuru Mwenyezi Mungu kwa hayo, bali wanamzulia Mwenyezi Mungu uwongo!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na hawa wanaomzulia Allah Mtukufu urongo, wakamnasibishia uharamishaji wa vitu ambavyo Yeye Hakuviharamisha kati ya riziki na vyakula, wanadhani kuwa Allah Mtukufu Atawafanya nini Siku ya Kiyama, siku ya wao kuhesabiwa, kwa urongo wao waliomzulia? Je,wanadhani kwamba Yeye Atawaacha na Atawasamehe? Allah Mtukufu Ana wema mwingi kwa viumbe Wake kwa kuacha Kwake kuyaharakisha mateso duniani kwa aliyemzulia urongo, na badala yake kumpa muhula. Lakini wengi zaidi wa watu hawamshukuru Allah Mtukufu kwa wema wake juu yao kwa hilo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yunus

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net