Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 10 · Aya ya 59

Yunus 10:59

يونس

قُلْ أَرَءَيْتُم مَّآ أَنزَلَ ٱللَّهُ لَكُم مِّن رِّزْقٍ فَجَعَلْتُم مِّنْهُ حَرَامًا وَحَلَـٰلًا قُلْ ءَآللَّهُ أَذِنَ لَكُمْ ۖ أَمْ عَلَى ٱللَّهِ تَفْتَرُونَ

Maana

Sema: Je, mnaonaje yale aliyowateremshia Mwenyezi Mungu katika riziki, basi mkafanya katika hizo nyingine haramu na nyingine halali. Sema, "Je, Mwenyezi Mungu aliwaruhusu, au mnamzulia Mwenyezi Mungu tu?"

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Sema: je, mwaonaje zile rizki alizo kutemshieni Mwenyezi Mungu nanyi makafanya katika hizo nyingine haramu na nyingine halali Sema: je, Mwenyezi Mungu amekuruhusuni au mnamzulia Mwenyezi Mungu tu. [59]

[59] Ewe Mtume! Waambie makafiri walio pewa baadhi ya starehe za duniani: Niambieni khabari ya vyakula vizuri vya halali alivyo kuruzukuni Mwenyezi Mungu, mkajifanya wenyewe ni watungaji sharia, mkahalalisha vingine na mkaharimisha vingine, bila ya kufuata Sharia ya Mwenyezi Mungu! Hakika Mwenyezi Mungu hakukupeni ruhusa mfanye hayo, bali nyinyi mnamzulia uwongo Mwenyezi Mungu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Sema, ewe Mtume, kuwaambia hawa wanaokataa wahyi, «Nipeni habari juu ya hii riziki ya wanyama, mimea na vitu vizuri ambavyo Allah Mtukufu Amewaumbia nyinyi, mkajihalalishia baadhi ya hivyo na mkajiharamishia vinginevyo.» Waambie, «Je, Allah Mtukufu Amewaruhusu hilo au mnaongea maneno ya ubatilifu ya kumzulia Allah Mtukufu na mnasema urongo?» Hakika wao wanaongea maneno ya ubatilifu ya kumzulia Allah Mtukufu na wanasema urongo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yunus

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net