Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 10 · Aya ya 58

Yunus 10:58

يونس

قُلْ بِفَضْلِ ٱللَّهِ وَبِرَحْمَتِهِۦ فَبِذَٰلِكَ فَلْيَفْرَحُوا۟ هُوَ خَيْرٌ مِّمَّا يَجْمَعُونَ

Maana

Sema, "Kwa fadhila ya Mwenyezi Mungu na rehema yake! Basi na wafurahi kwa hayo. Hayo ndiyo bora kuliko hayo wanayoyakusanya."

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Sema: Kwa fadhila ya Mwenyezi Mungu na rehema yake! Basi nawafurahi kwa hayo. Haya ni bora kuliko hayo wanayo yakusanya. [58]

[58] Ewe Mtume! Waambie: Furahieni fadhila ya Mwenyezi Mungu na rehema yake juu yenu kwa kuiteremsha Qur'ani, na kubainisha Sharia ya Islamu. Na hii ni bora kuliko starehe zote anazo zikusanya mtu duniani, kwa sababu hichi ni chakula cha nyoyo na dawa ya maradhi yake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Sema, ewe Mtume, kuwaambia watu wote, «Kwa wema wa Allah Mtukufu na rehema Yake, basi na wawe na furaha.» Wema wa Allah Mtukufu na rehema Yake ni Uislamu ambao ni uongofu na ni Dini ya haki aliyokuja nayo Mtume, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie, kutoka kwa Allah Mtukufu. Kwani Uislamu ambao Allah Mtukufu Amewaita wao waufuate, na Qur’ani ambayo Aliiteremsha kwa Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie) ni bora kuliko taka za ulimwengu wanazozikusanya na anasa zilizomo ndani yake zenye kutoeka kuondoka.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yunus

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net