Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 10 · Aya ya 57

Yunus 10:57

يونس

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ قَدْ جَآءَتْكُم مَّوْعِظَةٌ مِّن رَّبِّكُمْ وَشِفَآءٌ لِّمَا فِى ٱلصُّدُورِ وَهُدًى وَرَحْمَةٌ لِّلْمُؤْمِنِينَ

Maana

Enyi watu! Yamekwishawajia mawaidha kutoka kwa Mola wenu Mlezi, na ponya ya yale yaliyo katika vifua, na uongofu, na rehema kwa Waumini.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Enyi watu! Yamekujieni mawaidha kutoka kwa Mola wenu Mlezi, na poza kuponyesha yaliyomo vifuani, na uwongofu, na rehema kwa Waumini. [57]

[57] Enyi watu! Kimekujieni kwa ulimi wa Mtume Muhammad Kitabu kilicho toka kwa Mwenyezi Mungu. Ndani yake mna makumbusho ya Imani, na ut'iifu, na mawaidha ya kuhimiza kheri, na kukataza vitendo viovu, na kueleza mzingatie khabari za walio kutangulieni, na kukutakeni muangalie utukufu wa uumbaji ili mpate kuuelewa utukufu wa Muumba. Na ndani ya Kitabu hicho mna dawa ya maradhi ya nyoyo zenu, maradhi ya shirki na unaafiki; na mna uwongofu wa kuendea Njia Iliyo Nyooka. Na yote hayo ni rehema kwa Waumini wanao itikia wito.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Enyi watu yamewajia nyinyi mawaidha kutoka kwa Mola wenu yanayowakumbusha mateso ya Allah Mtukufu na yanayowaonya makamio Yake, nayo ni Qur’ani na yale iliyoyakusanya ya miujiza na mawaidha ili kuzitengeneza tabia zenu na matendo yenu. Na ndani yake muna dawa ya yaliyomo nyoyoni ya ujinga na ushirikina na magonjwa mengineyo, na muna uongofu kwa viumbe wenye kuifuata iwaokoe na maangamivu. Allah Mtukufu, Aliyetukuka na kuwa juu, Ameijaalia ni neema na rehema kwa Waumini. Na Amewahusu Waumini kwa hilo, kwa kuwa wao ndio wenye kunufaika na Imani. Ama makafiri, hiyo Qur’ani kwao ni giza.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yunus

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net