Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 10 · Aya ya 56

Yunus 10:56

يونس

هُوَ يُحْىِۦ وَيُمِيتُ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ

Maana

Yeye ndiye anayehuisha na anayefisha. Na kwake mtarejeshwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Yeye ndiye anaye fufua na anaye fisha. Na kwake mtarejeshwa [56]

[56] Na Mwenyezi Mungu Subhanahu anavihuisha vitu baada ya kuwa havipo, na anaviondoa baada ya kuwapo. Na kwake Yeye tu ndio marejeo katika Akhera. Na mwenye kuwa hivyo hapana kuu la kumshinda.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika Allah Mtukufu Ndiye Mwenye kuhuisha na Mwenye kufisha, Hashindwi kuwahuisha watu baada ya kufa kwao, kama ambavyo hakumshindi Yeye kuwafisha Atakapo hilo. Na wao ni wenye kurejea Kwake baada ya kufa kwao.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yunus

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net