Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 10 · Aya ya 55

Yunus 10:55

يونس

أَلَآ إِنَّ لِلَّهِ مَا فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ ۗ أَلَآ إِنَّ وَعْدَ ٱللَّهِ حَقٌّ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ

Maana

Jueni kuwa hakika ni vya Mwenyezi Mungu vyote vilivyo katika mbingu na katika ardhi. Jueni kuwa hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya haki. Lakini wengi wao hawajui.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Jueni kuwa hakika vyote viliomo katika mbingu na katika ardhi ni vya Mwenyezi Mungu. Jueni kuwa hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya haki. Lakini wengi wao hawajui. [55]

[55] Watu nawajue kuwa hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kumiliki na Mwenye madaraka makuu juu ya vyote viliomo mbinguni na duniani. Na pia wajue kuwa ahadi yake ni ya kweli. Basi Yeye hashindwi na kitu, na hapana yeyote ataye epuka malipwa yake. Lakini wao wamedanganyika na maisha ya dunia, hawajui hayo kwa ujuzi wa yakini!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Jua utanabahi kwamba kila kilichoko mbinguni na ardhini ni milki ya Allah Mtukufu, Aliyetukuka, hakuna kitu chochote kati ya hivyo ni cha yoyote isipokuwa Yeye. Jua utanabahi kwamba kukutana na Allah Mtukufu kuko na adhabu Yake kwa washirikina ni yenye kuwa, lakini wengi wao hawaujui uhakika wa hilo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yunus

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net