Yunus 10:54
يونسوَلَوْ أَنَّ لِكُلِّ نَفْسٍ ظَلَمَتْ مَا فِى ٱلْأَرْضِ لَٱفْتَدَتْ بِهِۦ ۗ وَأَسَرُّوا۟ ٱلنَّدَامَةَ لَمَّا رَأَوُا۟ ٱلْعَذَابَ ۖ وَقُضِىَ بَيْنَهُم بِٱلْقِسْطِ ۚ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ
Na lau kuwa kila nafsi iliyodhulumu inamiliki kila kilichomo katika ardhi, basi bila ya shaka ingejikomboa kwavyo. Na watakapoiona adhabu, wataficha majuto. Na itahukumiwa baina yao kwa uadilifu, nao hawatadhulumiwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na lau kuwa kila nafsi iliyo dhulumu inamiliki kila kiliomo duniani,bila ya shaka ingeli toa vyote kujikombolea. Na watakapo iona adhabu wataficha majuto. Na patahukumiwa baina yao kwa uadilifu, nao hawatadhulumiwa. [54]
[54] Na lau kuwa vitu vyote viliomo duniani ni mali ya kila nafsi iliyo dhulumu kwa ushirikina na kukanusha, ingeli vitoa fidia kwa adhabu itayo wakabili Siku ya Kiyama, na ambayo wataviona vitisho vyake. Na hapo basi majuto na masikitiko yatawajaa nyoyoni mwao kwa kutoweza kuyatamka, na kwa fazaa itayo wapata kwa kuiona adhabu! Na hukumu ya Mwenyezi Mungu itapita juu yao kwa uadilifu, na wala hawatodhulumiwa katika malipo hayo, kwani hayo ni matokeo ya waliyo yatenda duniani!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na lau kwamba kila nafsi iliyomshirikisha na kumkanusha Allah Mtukufu itakuwa na vyote vilivyomo ardhini, na ikaweza kuvifanya ni fidia yake ya kujikomboa na adhabu hiyo, ingalijikomboa kwavyo. Na wale ambao walidhulumu wataficha majuto yao watakapoiona adhabu ya Allah Mtukufu imewashukia wao wote. Na Allah Mtukufu, Aliyetukuka na kuwa juu, Atahukumu baina yao kwa uadilifu, na wao hawatadhulumiwa, kwa kuwa Allah Mtukufu, Hamuadhibu yoyote isipokuwa kwa dhambi zake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net