Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 10 · Aya ya 53

Yunus 10:53

يونس

وَيَسْتَنۢبِـُٔونَكَ أَحَقٌّ هُوَ ۖ قُلْ إِى وَرَبِّىٓ إِنَّهُۥ لَحَقٌّ ۖ وَمَآ أَنتُم بِمُعْجِزِينَ

Maana

Na wanakuuliza, "Je, ni kweli hayo?" Sema, "Ehe! Ninaapa kwa Mola wangu Mlezi! Hakika hayo ni kweli, na wala nyinyi hamtashinda."

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wanakuuliza: Je! Ni kweli hayo? Sema: Ehe! Naapa kwa Mola wangu Mlezi! Hakika hayo ni kweli, na wala nyinyi hamshindi! [53]

[53] Na makafiri, kwa njia ya kejeli na kukataa, wanakutaka wewe, Mtume, uwaambie hivyo ni kweli hayo uliyo yaleta katika Qur'ani na khabari za kufufuliwa, na adhabu? Waambie: Naam! Kwa haki ya Muumba wangu aliye niumba, hakika hayo yatakuwa bila ya shaka yoyote. Wala nyinyi hamtoshinda wala hamwezi kuzuia adhabu aitakayo Mwenyezi Mungu kukuleteeni.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na hao washirikina miongoni mwa watu wako, ewe Mtume, wanataka uwape habari kuhusu adhabu Siku ya Kiyama, Je, ni kweli hiyo? Waambie, ewe Mtume, Ndio, naapa kwa Mola wangu, hiyo ni kweli isiokuwa na shaka.Na nyinyi si wenye kumlemea Allah Mtukufu Asiwafufue na kuwalipa, kwani nyinyi muko kwenye udhibiti wa Allah Mtukufu na mamlaka Yake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yunus

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net