Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 10 · Aya ya 64

Yunus 10:64

يونس

لَهُمُ ٱلْبُشْرَىٰ فِى ٱلْحَيَوٰةِ ٱلدُّنْيَا وَفِى ٱلْـَٔاخِرَةِ ۚ لَا تَبْدِيلَ لِكَلِمَـٰتِ ٱللَّهِ ۚ ذَٰلِكَ هُوَ ٱلْفَوْزُ ٱلْعَظِيمُ

Maana

Wao wana bishara njema katika uhai wa dunia na katika Akhera. Hakuna mabadiliko katika maneno ya Mwenyezi Mungu. Huko ndiko kufuzu kukubwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wao wana bishara njema katika maisha ya dunia na katika Akhera. Hapana mabadiliko katika maneno ya Mwenyezi Mungu. Huko ndiko kufuzu kukubwa. [64]

[64] Kwa wapenzi hawa wa Mwenyezi Mungu pana bishara ya kheri hapa duniani, kwa vile Mwenyezi Mungu amewaahidi kuwapa ushindi na utukufu, na Akhera itatimia ahadi ya Mwenyezi Mungu. Na ahadi ya Mwenyezi Mungu haigeuki. Na haya ndiyo waliyo bashiriwa kwayo duniani, na watayapata Akhera. Na huko ndiko kufuzu kukubwa.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Mawalii hawa wana bishara njema kutoka kwa Allah Mtukufu kuwa watapata ya kuwafurahisha katika maisha ya kilimwengu, na miongoni mwayo ni ndoto njema anayoiona mwenyewe au akaonewa na duguye, na watapata Pepo kesho Akhera. Allah Mtukufu Haendi kinyume na ahadi Yake wala Haigeuzi. Huko ndiko kufaulu kukubwa, kwa kuwa bishara hiyo imekusanya kuokoka na kila lifanyiwalo hadhari na kufaulu kupata kila litakwalo na kupendwa.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yunus

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net