Yunus 10:50
يونسقُلْ أَرَءَيْتُمْ إِنْ أَتَىٰكُمْ عَذَابُهُۥ بَيَـٰتًا أَوْ نَهَارًا مَّاذَا يَسْتَعْجِلُ مِنْهُ ٱلْمُجْرِمُونَ
Sema, “Mnaonaje ikiwajia adhabu yake hiyo usiku au mchana. Basi wahalifu wanaharakisha nini?”
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Sema: Mwaonaje ikikufikieni hiyo adhabu yake usiku au mchana, sehemu gani ya adhabu wanaihimiza wakosefu? [50]
[50] Waambie wanao himiza ifike adhabu: Hebu niambieni, ikikufikieni adhabu ya Mwenyezi Mungu usiku au mchana, pana faida gani watayo ipata wakosefu wenye madhambi kutaka ije kwa haraka? Na hali adhabu yote ni mbaya!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Sema, ewe Mtume, kuwaambia hawa washirikina, «Nipeni habari ikiwajia adhabu ya Allah Mtukufu mchana au usiku, ni kitu gani mnachokifanyia haraka, enyi wahalifu, kuwa adhabu iteremke?»
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net