Yunus 10:49
يونسقُل لَّآ أَمْلِكُ لِنَفْسِى ضَرًّا وَلَا نَفْعًا إِلَّا مَا شَآءَ ٱللَّهُ ۗ لِكُلِّ أُمَّةٍ أَجَلٌ ۚ إِذَا جَآءَ أَجَلُهُمْ فَلَا يَسْتَـْٔخِرُونَ سَاعَةً ۖ وَلَا يَسْتَقْدِمُونَ
Sema: Sijimilikii nafsi yangu shari wala kheri ila apendavyo Mwenyezi Mungu. Kila umma una muda wao waliowekewa. Ukifika muda wao, hawakawii hata saa moja wala hawatangulii.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Sema: Sijimilikii nafsi yangu shari wala kheri ila apendavyo Mwenyezi Mungu. Kila umma una muda wao walio wekewa. Ukifika muda wao hawakawii hata saa moja wala hawatangulii. [49]
[49] Ewe Mtume! Waambie: Mimi sina uwezo wa kujitendea mwenyewe kheri wala shari, ila kwa aliyo niwezesha Mwenyezi Mungu. Basi vipi niweze kuihimiza ije upesi hiyo adhabu? Hakika kila umma una ukomo wake aliyo uwekea Mwenyezi Mungu tangu na tangu. Ukiwadia ukomo huo basi hawatoweza kuuchelewesha hata kidogo, kama wasivyo weza kuutanguliza!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Waambie, ewe Mtume, Siwezi kuiepushia nafsi yangu madhara wala kuiletea manufaa isipokuwa Akiwa Allah Mtukufu Ametaka kuniepushia madhara au kuniletea manufaa. Kila watu wana wakati wa kumalizika muda wao na kipindi chao cha kuishi, basi ujapo wakati wa kumalizika kipindi chao cha kuishi na kukoma umri wao, hawatachelewa hata kwa muhula wa saa moja wala hautatangulia muda wa maisha yao mbele ya wakati maalumu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net