Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 10 · Aya ya 48

Yunus 10:48

يونس

وَيَقُولُونَ مَتَىٰ هَـٰذَا ٱلْوَعْدُ إِن كُنتُمْ صَـٰدِقِينَ

Maana

Na wanasema, “Ni lini ahadi hii, ikiwa nyinyi ni wakweli?"

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

. Na wanasema: Lini ahadi hii, ikiwa mnasema kweli? [48]

[48] Na makafiri wanakusudia kuikanusha Siku ya Akhera, basi wanaihimiza kwa kejeli na kusema: Itakuwa lini hiyo adhabu unayo tuahidi, kama wewe, ewe Mtume, na hao walio pamoja nawe, ni wakweli katika hayo mnayo yaamini na mnatuitia sisi tuyakubali?

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na washirikina katika watu wako, ewe Mtume, wanasema, «Ni lini kitasimama Kiyama iwapo wewe na waliokufuata ni miongoni mwa wakweli katika yale mnayotuahidi kwayo?»

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yunus

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net