Yunus 10:47
يونسوَلِكُلِّ أُمَّةٍ رَّسُولٌ ۖ فَإِذَا جَآءَ رَسُولُهُمْ قُضِىَ بَيْنَهُم بِٱلْقِسْطِ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ
Na kila umma una Mtume. Kwa hivyo, anapowajia Mtume wao, inahukumiwa baina yao kwa uadilifu, nao hawadhulumiwi.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na kila umma una Mtume. Alipo wajia Mtume wao walihukumiwa baina yao kwa uadilifu, wala hawakudhulumiwa. [47]
[47] Na kila umma ulijiwa na Mtume akafikisha wito wa Mwenyezi Mungu, akaamini aliye amini, na akakanusha aliye kanusha. Ikifika Siku ya kufufuliwa, Mtume wao atakuja na kuwatolea ushahidi wale walio mkadhibisha kuwa hao ni makafiri, na walio amini kuwa ni Waumini. Basi Mwenyezi Mungu atawahukumu kwa uadilifu ulio timia. Hatomdhulumu yeyote katika malipo anayo stahiki.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na kila ummah uliopita kabla yenu, enyi watu, ulikuwa na mjumbe niliyemtuma kwao, kama nilivyomtuma Muhammad kwenu Alinganie kwenye Dini ya Allah Mtukufu na kuwa na utiifu Kwake. Basi huyo mjumbe wao atakapokuja Akhera, hapo kutaamuliwa baina yao kwa uadilifu, na wao hawatadhulumiwa katika malipo ya matendo yao chochote.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net