Yunus 10:46
يونسوَإِمَّا نُرِيَنَّكَ بَعْضَ ٱلَّذِى نَعِدُهُمْ أَوْ نَتَوَفَّيَنَّكَ فَإِلَيْنَا مَرْجِعُهُمْ ثُمَّ ٱللَّهُ شَهِيدٌ عَلَىٰ مَا يَفْعَلُونَ
Na ima tutakuonyesha baadhi ya yale tunayowaahidi, au tukufishe kabla yake, basi marejeo yao ni kwetu. Kisha Mwenyezi Mungu ni Shahidi wa wanayoyafanya.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na vyovyote vile, tukikuonyesha baadhi ya tunayo waahidi, au tukakufisha kabla yake, marejeo yao ni kwetu. Kisha Mwenyezi Mungu ni Shahidi wa wanayo yafanya. [46]
[46] Ewe Mtume! Tukikuonyesha baadhi ya tunayo waahidi, nayo kuwa utawashinda na wao watapata adhabu, au tukakufisha kabla ya kuyaona yote hayo, vyovyote vile hawawezi kuepuka kurejea kwetu tuwahisabie na kuwalipa. Na Mwenyezi Mungu Subhanahu ni Mwenye kuwachungua na Mwenye kujua kila walitendalo, naye atawalipa.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na iwapo tutakuonesha, ewe Mtume, katika uhai wako baadhi ya mateso tunayowaahidi duniani, au tukakufisha kabla hatujakuonesha hayo kwao, ni kwetu sisi peke yetu marejeo ya mambo yao katika hali zote mbili, kisha Allah Mtukufu ni Shahidi wa vitendo vyao waliokuwa wakivifanya duniani, hakuna chochote kati ya hivyo kinafichika Kwake, na Atawalipa malipo yao wanayostahiki kwa vitendo vyao hivyo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net