Yunus 10:45
يونسوَيَوْمَ يَحْشُرُهُمْ كَأَن لَّمْ يَلْبَثُوٓا۟ إِلَّا سَاعَةً مِّنَ ٱلنَّهَارِ يَتَعَارَفُونَ بَيْنَهُمْ ۚ قَدْ خَسِرَ ٱلَّذِينَ كَذَّبُوا۟ بِلِقَآءِ ٱللَّهِ وَمَا كَانُوا۟ مُهْتَدِينَ
Na Siku atakapowakusanya, itakuwa kama kwamba hawakukaa isipokuwa saa moja tu katika mchana! Watatambuana. Hakika wamehasirika wale waliokadhibisha kukutana na Mwenyezi Mungu, wala hawakuongoka.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na Siku atakapo wakusanya, itakuwa kama kwamba hawakukaa ila saa moja tu ya mchana! Watatambuana. Hakika wamekhasirika walio kanusha kukutana na Mwenyezi Mungu, wala hawakuwa wenye kuongoka. [45]
[45] Ewe Mtume! Wahadharishe na Siku tutayo wakusanya kwa ajili ya Hisabu, wawe na hakika kuwa Siku ya Akhera itakuja, baada ya kuwa walikuwa wakiikanusha na wakikumbuka maisha yao ya duniani tu. Waone ni kama saa moja tu ya mchana, hapana wasaa wa kufanya kitendo chochote cha kheri, na wajuane wao kwa wao wakilaumiana kwa kufuru na upotovu walio kuwa nao! Wamekhasiri wakanushao Siku ya Akhera na wasitangulize vitendo vyema katika dunia yao, na wakakosa neema za Akhera kwa kufuru zao.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na siku Allah Mtukufu Atawakusanya washirikina hawa, Siku ya kufufuliwa na kuhesabiwa, kama kwamba wao kabla ya hapo hawakukaa katika maisha ya duniani isipokuwa kadiri ya muda mchache wa kipindi cha mchana, watajuana wao kwa wao kama walivyokuwa duniani, kisha kujuana huko kutakatika na muda huo utapita. Hakika wamepata hasara wale waliokataa na kukanusha kuwa watakutana na Allah Mtukufu na kuwa Ana thawabu na Ana adhabu. Na hawakuwa ni wenye kuafikiwa kupata uongofu katika yale waliyoyafanya.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net