Yunus
Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.
Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22
وَيَوْمَ يَحْشُرُهُمْ كَأَن لَّمْ يَلْبَثُوٓا۟ إِلَّا سَاعَةً مِّنَ ٱلنَّهَارِ يَتَعَارَفُونَ بَيْنَهُمْ ۚ قَدْ خَسِرَ ٱلَّذِينَ كَذَّبُوا۟ بِلِقَآءِ ٱللَّهِ وَمَا كَانُوا۟ مُهْتَدِينَ 45
{45} Yeye Mtukufu anajulisha juu ya dunia kuisha haraka kwa dunia, na kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu atakapowakusanya watu na akawajumuisha katika siku ambayo hakuna shaka juu yake, itakuwa ni kana kwamba hawakukaa isipokuwa saa moja tu katika mchana, na kana kwamba hawakupitiwa na furaha wala taabu. Nao watatambuana kama ilivyokuwa hali yao katika dunia hii. Na katika Siku hii wachamungu watapata faida, na watahasirika “wale waliokadhibisha kukutana na Mwenyezi Mungu, wala hawakuongoka,” kwenye njia iliyonyooka, na Dini madhubuti kwa maana walikosa starehe, na wakastahiki kuingia Motoni.