Yunus 10:51
يونسأَثُمَّ إِذَا مَا وَقَعَ ءَامَنتُم بِهِۦٓ ۚ ءَآلْـَٔـٰنَ وَقَدْ كُنتُم بِهِۦ تَسْتَعْجِلُونَ
Tena je, ikishatokea ndiyo mtaiamini? Je, sasa? Na ilhali mlikuwa mkiifanyia haraka?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Tena je! Ikisha tokea mtaiamini? Je! Ndio sasa tena? Na nyinyi mlikuwa mkiihimiza. [51]
[51] Sasa mnaikanusha adhabu? Tena itapo kufikieni mtaambiwa kwa kubeuliwa: Je! Sasa mnaamini kwa kuwa mnaiona, na nyinyi huko duniani mlikuwa mkiihimiza kwa dharau na kukanusha!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Je, baada ya kushuka adhabu ya Allah Mtukufu kwenu, enyi washirikina, ndipo mtaamini, wakati ambapo Imani haitawafaa? Wakati huo mtaambiwa, ‘Je, sasa ndipo mnaamini na hapo nyuma mlikuwa mnaifanyia haraka?’
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net