Yunus 10:34
يونسقُلْ هَلْ مِن شُرَكَآئِكُم مَّن يَبْدَؤُا۟ ٱلْخَلْقَ ثُمَّ يُعِيدُهُۥ ۚ قُلِ ٱللَّهُ يَبْدَؤُا۟ ٱلْخَلْقَ ثُمَّ يُعِيدُهُۥ ۖ فَأَنَّىٰ تُؤْفَكُونَ
Sema: Je, yupo katika washirika wenu mwenye kuanzisha kuumba viumbe, kisha akavirejesha? Sema: Mwenyezi Mungu anaanzisha kuumba viumbe, kisha anavirejesha. Basi ni vipi mnadanganywa?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Sema: Je! Yupo katika miungu yenu ya ushirikina aliye anzisha kuumba viumbe, na kisha akavirejesha? Huwaje, basi, mkadanganywa? [34]
[34] Ewe Mtume! Waambie hao washirikina: Yupo yeyote katika hao mlio wafanya washirika wa Mwenyezi Mungu mkawaabudu, awezaye kuanzisha kuumba tangu mwanzo, na tena akarejea tena baada ya kwisha toweka? Hapana shaka watashindwa kujibu! Basi hapo tena waambie: Allah, Mwenyezi Mungu, tu peke yake, ndiye anaye anzisha kuumba kutokana na kuto kuwepo, na tena viumbe vikitoweka huvirejesha. Vipi basi nyinyi mnaiacha Imani?
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Sema, ewe Mtume, kuwaambia wao, «Je, kuna yoyote, miongoni mwa waungu wenu na waabudiwa wenu, mwenye kuanzisha kuumba chochote kisicho na asili (ya mfano uliotangulia) kisha akifanye kitoweke baada ya kukianzisha, kisha akirudishe kama namna kilivyokuwa kabla hajakifanya kitoweke?» Kwa hakika, wao hawawezi kufanya madai hayo. Sema, ewe Mtume, «Allah Mtukufu, Peke Yake, Ndiye Anayeanzisha kuumba kisha Akakifanya kitoweke kile Alichokiumba, kisha Akakirudisha. Basi ni vipi nyinyi mnajiepusha na njia ya haki na kufuata ubatilifu, nao ni kumuabudu asiyekuwa Allah Mtukufu?»
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net