Yunus 10:33
يونسكَذَٰلِكَ حَقَّتْ كَلِمَتُ رَبِّكَ عَلَى ٱلَّذِينَ فَسَقُوٓا۟ أَنَّهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ
Ndivyo hivyo kauli ya Mola wako Mlezi ilivyowathibitikia wale waliovuka mipaka ya kwamba hawataamini.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Ndio kama hivyo kauli ya Mola wako Mlezi itakavyo wathibitikia wale walio potoka, ya kwamba hawatoamini. [33]
[33] Kama ulivyo thibiti Ungu wa Mwenyezi Mungu na kumuabudu Yeye, vile vile imethibiti hukumu juu ya walio tokana na amri ya Mwenyezi Mungu wakimuasi kwa kuwa hawaifuati Haki. Kwani hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu hawaongoi kwenye Haki ila wanao ishika njia yake, sio wanao mfanyia uasi.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Kama walivyokanusha washirikina hawa na walivyoendelea kwenye ushirikina wao, ndivyo lilivothibiti neno la Mola wako, hukumu Yake na uamuzi Wake juu ya wale waliotoka nje ya utiifu Wake wakaenda kumuasi na wakamkanusha, kwamba wao hawataamini upweke wa Allah Mtukufu wala unabii wa Nabii Wake Muhammad, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie, wala hawatafanya matendo yanayolingana na uongofu Wake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net