Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 10 · Aya ya 32

Yunus 10:32

يونس

فَذَٰلِكُمُ ٱللَّهُ رَبُّكُمُ ٱلْحَقُّ ۖ فَمَاذَا بَعْدَ ٱلْحَقِّ إِلَّا ٱلضَّلَـٰلُ ۖ فَأَنَّىٰ تُصْرَفُونَ

Maana

Basi huyo ndiye Mwenyezi Mungu, Mola wenu Mlezi wa haki. Na kipo kitu gani baada ya haki, isipokuwa upotovu tu? Basi ni vipi mnageuzwa?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Basi huyo ndiye Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wenu wa haki. Na kipo kitu gani baada ya haki, isipokuwa upotovu tu? Basi huwaje mkageuzwa? [32]

[32] Huyo basi ndiye Mwenyezi Mungu mliye mkiri, na Yeye tu peke yake ndiye Mola wenu Mlezi aliye thibiti kuwa ni Mola na Mlezi, na akapasa kuabudiwa pekee, wala hapana mwenginewe. Na hapana baada ya Haki ya Umoja wa Mwenyezi Mungu na kumuabudu Yeye tu, ila kutumbukia katika upotovu, nao ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu na kumuabudu mwenginewe. Basi vipi mnaiacha Haki mkauendea upotovu?

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Huyo Ndiye Allah Mtukufu Mola wenu! Yeye Ndiye kweli isiyo na shaka, Anayestahiki kuabudiwa Peke Yake, Asiye na Mshirika. Basi ni kitu gani kisichokuwa kweli isipokuwa ni upotevu? Basi vipi nyinyi mtaepushwa na kumuabudu Yeye muelekezwe kumuabudu asiyekuwa Yeye?

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yunus

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net