Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 10 · Aya ya 31

Yunus 10:31

يونس

قُلْ مَن يَرْزُقُكُم مِّنَ ٱلسَّمَآءِ وَٱلْأَرْضِ أَمَّن يَمْلِكُ ٱلسَّمْعَ وَٱلْأَبْصَـٰرَ وَمَن يُخْرِجُ ٱلْحَىَّ مِنَ ٱلْمَيِّتِ وَيُخْرِجُ ٱلْمَيِّتَ مِنَ ٱلْحَىِّ وَمَن يُدَبِّرُ ٱلْأَمْرَ ۚ فَسَيَقُولُونَ ٱللَّهُ ۚ فَقُلْ أَفَلَا تَتَّقُونَ

Maana

Sema, "Ni nani anayekuruzukuni kutoka mbinguni na ardhini? Au ni nani anayemiliki kusikia na kuona? Na ni nani atoaye kilicho hai kutoka kwa maiti, na atoaye maiti kutoka kwa kilicho hai? Na ni nani anayeyaendesha mambo yote?" Basi watasema, "Mwenyezi Mungu." Basi sema, "Je, hamchi?"

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Sema: Ni nani anaye kuruzukuni kutoka mbinguni na kwenye ardhi? Au ni nani anaye miliki kusikia na kuona? Na nani amtoaye hai kutoka maiti, na akamtoa maiti kutoka aliye hai? Na nani anaye yadabiri mambo yote? Watasema:Allah, Mwenyezi Mungu. Basi sema: Je! Hamchi? [31]

[31] Ewe Mtume! Lingania kwenye Tawhidi safi, na useme: Nani anaye kuleteeni riziki kutoka mbinguni inapo teremka mvua, na katika ardhi inapo mea mimea na kuzaa? Na nani aliye kupeni kusikia na kuona? Na nani anaye toa vilio hai kutokana na vilio maiti, kama mimea, nayo ni hai kutokana na ardhi maiti? Nani anaye mtoa maiti kutokana na hai, kama mtu anavyo kufa? Na nani anaye panga na kuendesha mambo yote ya ulimwengu kwa kudra yake na hikima yake? Wataungama: Hapana pa kukimbilia! Kwa hakika ni Mwenyezi Mungu peke yake ndiye mtenda yote. Ewe Mtume! Waambie watapo ungama: Si waajibu mkubwa kuit'ii Haki, na kumkhofu Mwenyezi Mungu, Mmiliki Ufalme wote?

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Waambie, ewe Mtume, washirikina hawa, «Ni nani anayewaruzuku kutoka juu kwa mvua anayoiteremsha, na kutoka ardhini kwa mimea na miti aina mbalimbali anayoiotesha kutoka humo, ambayo miongoni mwayo mnakula nyinyi na wanyama wenu? Na ni nani anayemiliki hisia za kusikia na za kuona mnazostarehea, nyinyi na wengineo? Na ni nani anayemiliki uhai na kifo, katika ulimwengu wote, akawatoa wenye uhai na wafu, baadhi yao kutoka kwa wengine, katika viumbe mnavyovijua na msivyovijua? Na ni nani anayeyaendesha mambo ya mbinguni na ardhini na yaliyomo ndani yake, (anayeyaendesha) mambo yenu nyinyi na mambo ya viumbe vyote?» Watakujibu kwamba anayefanya yote hayo ni Allah Mtukufu. Waambie, «Basi si muogope mateso ya Allah Mtukufu mnapomuabudu mwingine pamoja na Yeye?»

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yunus

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net