Yunus 10:30
يونسهُنَالِكَ تَبْلُوا۟ كُلُّ نَفْسٍ مَّآ أَسْلَفَتْ ۚ وَرُدُّوٓا۟ إِلَى ٱللَّهِ مَوْلَىٰهُمُ ٱلْحَقِّ ۖ وَضَلَّ عَنْهُم مَّا كَانُوا۟ يَفْتَرُونَ
Huko kila nafsi itayajua iliyoyatanguliza. Na watarudishwa kwa Mwenyezi Mungu, Mola wao wa haki, na yote ya uongo waliyokuwa wakiyazua yatawapotea.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Huko kila mtu atayajua aliyo yatanguliza. Na watarudishwa kwa Mwenyezi Mungu, Mola wao wa Haki, na yote waliyo kuwa wakiyazua yatawapotea. [30]
[30] Katika msimamo huo kila mtu atajua kheri gani au shari gani aliyo ifanya, na atalipwa malipo yake. Na hapo hao washirikina watayakinika kuwa kweli Mwenyezi Mungu ni Mmoja na wa pekee, Mwenye Haki. Na yote waliyo kuwa wakimzulia Mwenyezi Mungu yatavunjika.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Katika kisimamo hiko cha kuhesabiwa, kila nafsi itazipekua na kuziona hali zake na matendo yake, na italipwa kulingana na hayo: yakiwa ni mema atalipwa mema na yakiwa ni maovu atalipwa maovu. Na wote watarejeshwa kwa Allah Mtukufu Aliye Muamuzi Muadilifu. Hapo watu wa Peponi watatiwa Peponi, na watu wa Motoni watatiwa Motoni, na vitawaondokea washirikina vile ambavyo walikua wakiviabudu badala ya Allah Mtukufu kwa kumzulia Yeye urongo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net