Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 10 · Aya ya 29

Yunus 10:29

يونس

فَكَفَىٰ بِٱللَّهِ شَهِيدًۢا بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمْ إِن كُنَّا عَنْ عِبَادَتِكُمْ لَغَـٰفِلِينَ

Maana

Basi Mwenyezi Mungu anatosha kuwa ni shahidi baina yetu na nyinyi. Hakika sisi tulikuwa hatuna habari na ibada yenu."

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Mwenyezi Mungu anatosha kuwa ni shahidi baina yetu na nyinyi. Hakika sisi tulikuwa hatuna khabari ya ibada yenu. [29]

[29] Mwenyezi Mungu anatutosheleza kwa ilimu yake na hukumu yake kuwa ni Shahidi wa kutupambanua baina yetu na nyinyi. Sisi tulikuwa mbali nanyi, wala hatukuwa tunafaidika vyovyote kwa huko kutuabudu kwenu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Basi yatosha kuwa Allah Mtukufu ni Shahidi baina yetu na nyinyi. Hakika sisi hatukuwa tunayajua yale mliokuwa mkiyafanya. Na hakika sisi tulikuwa ni wenye kughafilika kuwa nyinyi mnatuabudu, hatukuwa tunalihisi hilo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yunus

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net