Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 10 · Aya ya 28

Yunus 10:28

يونس

وَيَوْمَ نَحْشُرُهُمْ جَمِيعًا ثُمَّ نَقُولُ لِلَّذِينَ أَشْرَكُوا۟ مَكَانَكُمْ أَنتُمْ وَشُرَكَآؤُكُمْ ۚ فَزَيَّلْنَا بَيْنَهُمْ ۖ وَقَالَ شُرَكَآؤُهُم مَّا كُنتُمْ إِيَّانَا تَعْبُدُونَ

Maana

Na siku tutakapowakusanya wote, kisha tutawaambia wale walioshirikisha, "Simameni mahali penu nyinyi na washirika wenu." Kisha tutatenganisha baina yao. Na hao washirika wao watasema, "Nyinyi hamkuwa mkituabudu sisi.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na siku tutakapo wakusanya wote, kisha tutawaambia walio shirikisha:Simameni mahali penu nyinyi na wale mlio wafanya washirika. Kisha tutawatenga baina yao. Na hao walio washirikisha watasema: Nyinyi hamkuwa mkituabudu sisi. [28]

[28] Ewe Mtume! Kumbuka kitisho cha siku watapo kusanywa viumbe vyote, kisha tuwaambie walio mshirikisha Mwenyezi Mungu katika ibada zao: Simameni pahala penu nyinyi na hao mlio wafanya washirika wa Mwenyezi Mungu, muangalie mtafanywa nini? Patatokea mfarakano baina ya washirikina na hao miungu yao ya uwongo walio washirikisha na Mwenyezi Mungu. Hao miungu watajitenga na wale wafwasi wao, kwa kusema: Sisi hatukukutakeni mtuabudu. Wala nyinyi hamkuwa mkituabudu sisi! Hakika mlikuwa mkiyaabudu matamanio yenu tu!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kumbuka, ewe Mtume, Siku ambayo tutawafufua viumbe wote ili wahesabiwe na walipwe, kisha tuseme kuwaambia waliomshirikisha Allah Mtukufu, «Jilazimisheni mahali mliopo, nyinyi na washirika wenu ambao mlikuwa mkiwaabudu badala ya Allah Mtukufu, mpaka tuangalie mtafanya nini.» Hapo tutapambanua baina ya washirikina na wale wanaowaabudu, na watajitenga, wale walioabudiwa badala ya Allah Mtukufu, na wale waliokuwa wanawaabudu, na watasema kuwaambia washirikina «Hamkuwa mkituabudu sisi ulimwenguni».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yunus

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net