Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 10 · Aya ya 27

Yunus 10:27

يونس

وَٱلَّذِينَ كَسَبُوا۟ ٱلسَّيِّـَٔاتِ جَزَآءُ سَيِّئَةٍۭ بِمِثْلِهَا وَتَرْهَقُهُمْ ذِلَّةٌ ۖ مَّا لَهُم مِّنَ ٱللَّهِ مِنْ عَاصِمٍ ۖ كَأَنَّمَآ أُغْشِيَتْ وُجُوهُهُمْ قِطَعًا مِّنَ ٱلَّيْلِ مُظْلِمًا ۚ أُو۟لَـٰٓئِكَ أَصْحَـٰبُ ٱلنَّارِ ۖ هُمْ فِيهَا خَـٰلِدُونَ

Maana

Na wale waliochuma mabaya, malipo ya baya ni kwa mfano wake, na watafunikwa na madhila. Hawatakuwa na wa kuwalinda kutokana na Mwenyezi Mungu. Nyuso zao ni kama kwamba zimefunikwa na vipande vya usiku wa giza. Hao ndio watu wa Motoni. Wao, humo watadumu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wale walio chuma maovu, malipo ya uovu ni mfano wake vile vile, na yatawafika madhila. Hawatakuwa na wa kuwalinda na Mwenyezi Mungu. Nyuso zao kama kwamba zimefunikwa na vipande vya usiku wa giza. Hao ndio watu wa Motoni, wao humo watadumu. [27]

[27] Na wale ambao hawakuitikia Wito wa Mwenyezi Mungu, wakakufuru, wakatenda maasi, watalipwa kwa mujibu ya uovu walio utenda. Na hawana mlinzi wa kuwakinga na adhabu ya Mwenyezi Mungu. Na nyuso zao zitasawajika kwa ghamu na huzuni kama kwamba zimefunikwa na weusi wa kiza cha usiku! Na hao ndio watu wa Motoni, watasononeka humo milele.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na wale waliofanya maovu ulimwenguni, wakakanusha na wakamuasi Allah Mtukufu, watapata mateso ya Allah Mtukufu huko Akhera ambayo ni malipo yanayofanana na matendo yao maovu waliyoyafanya, na watafinikwa na unyonge na utwevu. Na hawatapata yoyote mwenye kuzuia adhabu ya Allah Mtukufu isiwafikie Akitaka kuwatesa. Nyuso zao zitakuwa ni kama zilizovishwa sehemu za weusi wa usiku wenye giza. Hawa ndio watu wa Motoni wenye kukaa milele humo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yunus

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net