Yunus 10:26
يونسلِّلَّذِينَ أَحْسَنُوا۟ ٱلْحُسْنَىٰ وَزِيَادَةٌ ۖ وَلَا يَرْهَقُ وُجُوهَهُمْ قَتَرٌ وَلَا ذِلَّةٌ ۚ أُو۟لَـٰٓئِكَ أَصْحَـٰبُ ٱلْجَنَّةِ ۖ هُمْ فِيهَا خَـٰلِدُونَ
Kwa wafanyao uzuri, ni uzuri na zaidi. Wala vumbi halitawafunika nyuso zao, wala madhila. Hao ndio watu wa Bustanini. Wao, humo watadumu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Kwa wafanyao wema ni wema na zaidi. Wala vumbi halitawafunika nyuso zao, wala madhila. Hao ndio watu wa Peponi. Humo watadumu. [26]
[26] Wanao tenda mema kwa kuitikia Wito wa Mwenyezi Mungu, wakaamini na wakafanya kheri kwa Dini yao na dunia yao, hao watapata wema katika Akhera, na wema huo ni Pepo. Na tena watapata yaliyo zidi hayo kwa fadhila na ukarimu wa Mwenyezi Mungu. Wala nyuso zao hazitafunikwa na huzuni na hamu na fedheha. Hawa ndio watu wa Peponi watakao neemeka humo daima milele.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Ni ya Waumini, waliofanya vizuri kumuabudu Allah Mtukufu,wakamtii katika yale Aliyowaamrisha na Akayakataza, Pepo na zaidi yake ambayo ni kuutazama Uso wa Allah Mtukufu, Aliyetukuka, huko Peponi, na kupata msamaha na radhi. Na wala nyuso zao hazitafinikwa na vumbi wala unyonge kama itakavyo kuwapata watu wa Moto. Hawa wanaosifika na sifa hizi ndio watu wa Peponi, ni wenye kukaa milele kabisa humo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net