Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 10 · Aya ya 25

Yunus 10:25

يونس

وَٱللَّهُ يَدْعُوٓا۟ إِلَىٰ دَارِ ٱلسَّلَـٰمِ وَيَهْدِى مَن يَشَآءُ إِلَىٰ صِرَٰطٍ مُّسْتَقِيمٍ

Maana

Na Mwenyezi Mungu anaita kwenye Nyumba ya amani, na anamwongoa amtakaye kwenye Njia iliyonyooka.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na Mwenyezi Mungu anaita kwendea Nyumba ya Amani, na anamwongoa amtakaye kwenye Njia Iliyo Nyooka. [25]

[25] Na Mwenyezi Mungu anawaitia waja wake kwa Imani na vitendo vyema wendee Peponi, makao ya amani na utulivu. Na Yeye Subhanahu humwongoa amtakaye - kwa kuwa kesha jitayarisha vyema na kaelekea kheri - kwenye Njia ya Haki, nayo ni ya Salama.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na Allah Mtukufu Anawaita kwenye mabustani ya Pepo Yake Aliyowaandalia wanaojitegemeza Kwake, na Anawaongoza Anaowataka miongoni mwa viumbe vyake, Akawaafikia kuipata njia iliyolingana sawa, nayo ni Uislamu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yunus

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net