Yunus 10:24
يونسإِنَّمَا مَثَلُ ٱلْحَيَوٰةِ ٱلدُّنْيَا كَمَآءٍ أَنزَلْنَـٰهُ مِنَ ٱلسَّمَآءِ فَٱخْتَلَطَ بِهِۦ نَبَاتُ ٱلْأَرْضِ مِمَّا يَأْكُلُ ٱلنَّاسُ وَٱلْأَنْعَـٰمُ حَتَّىٰٓ إِذَآ أَخَذَتِ ٱلْأَرْضُ زُخْرُفَهَا وَٱزَّيَّنَتْ وَظَنَّ أَهْلُهَآ أَنَّهُمْ قَـٰدِرُونَ عَلَيْهَآ أَتَىٰهَآ أَمْرُنَا لَيْلًا أَوْ نَهَارًا فَجَعَلْنَـٰهَا حَصِيدًا كَأَن لَّمْ تَغْنَ بِٱلْأَمْسِ ۚ كَذَٰلِكَ نُفَصِّلُ ٱلْـَٔايَـٰتِ لِقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ
Hakika mfano wa uhai wa dunia hii ni kama maji tuliyoyateremsha kutoka mbinguni, kisha mimea ya ardhi ikachanganyika nayo miongoni mwa vile wanavyovila watu na wanyama. Mpaka ardhi ilipokamilika uzuri wake, na ikapambika, na wenyewe wakadhani kwamba wameshaiweza, iliifikia amri yetu usiku au mchana, kwa hivyo tukaifanya kama iliyofyekwa, kama kwamba haikuwapo jana. Hivyo ndivyo tunavyozipambanua Ishara zetu kwa kaumu wanaotafakari.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hakika mfano wa maisha ya dunia ni kama maji tuliyo yateremsha kutoka mbinguni, kisha yakachanganyika na mimea ya ardhi wanayo ila watu na wanyama. Mpaka ardhi ilipo kamilika uzuri wake, na ikapambika, na wenyewe wakadhani wamesha iweza, iliifikia amri yetu usiku au mchana, tukaifanya kama iliyo fyekwa - kama kwamba haikuwapo jana. Namna hivi tunazipambanua Ishara zetu kwa watu wanao fikiri. [24]
[24] Hakika hali ya uhai wa dunia kwa uzuri wake na starehe zake, na kisha baada ya hayo kutoweka, si chochote ila ni kama hali ya maji yanayo teremka mbinguni, yakachanganyika na mimea ya ardhi inayo liwa na watu na wanyama. Mimea hiyo ikastawi na ikatoa matunda, na ardhi ikapambika kwa kunawiri. Uzuri huo ukisha fika ukomo wake, na wenyewe wakayakinika kuwa kweli ni mali yao, na kuwa watanafiika kwa matunda yake na neema zake, amri yetu ya kuondoa yote hayo ikaja. Tukaifanya kama kwamba iliyo fyekwa, na kama kwamba haijapata kukaliwa wala haikupata kuwa na uzuri kabla yake! Na hali zote mbili za kustawi na kunawiri ya kufurahia watu na kinyume cha hayo, ni mambo ya kuondoka na kutoweka! Na kama alivyo bainisha Mwenyezi Mungu kwa mifano iliyo wazi, anabainisha Aya zake na anafafanua hukumu zake na Ishara kwa watu wanao fikiri na wanapima kwa akili. Aya hii inaashiria ukweli ulio anza kuchomoza, nao ni kuwa mwanaadamu kwa kuifanya ilimu imtumikie ameweza kuyamiliki anayo yataka. Hata inapo kuwa karibu ya kufikilia ukweli huu kukamilika, na akaona huyo mwanaadamu amekwisha fikilia kilele cha ujuzi, hapo basi amri ya Mwenyezi Mungu hutokea.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakika mfano wa uhai wa kilimwengu na yale mnayojifahiri nayo baina yenu ya mapambo na mali ni kama mfano wa mvua tulioiteremsha kutoka juu kushuka ardhini, tukaotesha kwayo aina za mimea zilizochanganyika miongoni mwa zile zinazoliwa na watu katika matunda na zinazoliwa na wanyama katika nyasi, mpaka ulipoonekana wazi uzuri wa hii ardhi na mng’aro wake, na watu wa ardhi hii wakadhani kwamba wao ni waweza wa kuyavuna na kufaidika nayo, hapo amri yetu na hukumu yetu iliyajia kuwa ile mimea iliyoko juu yake iangamie na uzuri wake uondoke, kipindi cha usiku au mchana, tukaifanya mimea hii na miti imevunwa imekatwa, hakuna kitu katika ardhi hiyo, kama kwamba hapakuwa na mazao na mimea iliokuwa imesimama kabla ya hapo juu ya uso wa ardhi. Hivyo ndivyo kutoweka kunakomaliza yale mnayojigamba nayo baina yenu ya ulimwengu wenu na pambo lake, Allah Mtukufu Akayamaliza na kuyaangamiza. Na kama tulivyowafafanulia, enyi watu, mfano wa ulimwengu huu, na tukawajulisha uhakika wake, ndivyo tunavyofafanua hoja zetu na dalili zetu kwa watu wanaofikiri juu ya aya za Allah Mtukufu na wanaozingatia yanayowafaa duniani na Akhera.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net