Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 10 · Aya ya 23

Yunus 10:23

يونس

فَلَمَّآ أَنجَىٰهُمْ إِذَا هُمْ يَبْغُونَ فِى ٱلْأَرْضِ بِغَيْرِ ٱلْحَقِّ ۗ يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ إِنَّمَا بَغْيُكُمْ عَلَىٰٓ أَنفُسِكُم ۖ مَّتَـٰعَ ٱلْحَيَوٰةِ ٱلدُّنْيَا ۖ ثُمَّ إِلَيْنَا مَرْجِعُكُمْ فَنُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ

Maana

Lakini anapowaokoa, tazama, wanafanya jeuri tena katika ardhi bila ya haki. Enyi watu! Hakika jeuri zenu zitawadhuru nyinyi wenyewe. Hii ni starehe ya maisha ya dunia tu. Kisha marejeo yenu ni kwetu, na hapo tutawaambia yale mliyokuwa mkiyatenda.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Lakini akisha waokoa, mara wanafanya jeuri tena katika nchi bila ya haki. Enyi watu! Jeuri zenu zitakudhuruni wenyewe. Hii ni starehe ya maisha ya dunia tu. Kisha marejeo yenu ni kwetu, na hapo tutakuambieni mliyo kuwa mkiyatenda. [23]

[23] Na akisha waokoa kutokana na khatari ya kuteketea, wanavunja ahadi yao, na mara wanarejea kwenye fisadi walizo kuwa nazo kabla! Enyi watu mvunjao ahadi! Hakika matokeo ya kupindukia mipaka ya starehe na kudhulumu kwenu yatarejea juu yenu peke yenu. Na hakika hizo starehe mnazo zistarehea katika dunia yenu ni starehe za kidunia zenye mwisho. Kisha marejeo yenu ya mwisho ni kwa Mwenyezi Mungu, na Yeye atakulipeni kwa vitendo vyenu mlivyo vitanguliza duniani.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Allah Mtukufu Alipowaondolea shida na mikasa, punde si punde wakawa wanafanya uharibifu na maasia katika ardhi. Enyi watu, hakika ukorofi wa udhalimu wenu unawarudia nyinyi wenyewe. Chukueni starehe katika uhai wa kilimwengu wenye kuondoka, kisha kwetu ndio mwisho wenu na marejeo yenu, hapo tutawapa habari ya matendo yenu yote na tutawahesabu juu ya hayo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yunus

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net