Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 10 · Aya ya 109

Yunus 10:109

يونس

وَٱتَّبِعْ مَا يُوحَىٰٓ إِلَيْكَ وَٱصْبِرْ حَتَّىٰ يَحْكُمَ ٱللَّهُ ۚ وَهُوَ خَيْرُ ٱلْحَـٰكِمِينَ

Maana

Na wewe fuata yale yanayofunuliwa kwako kwa ufunuo (wahyi). Na vumilia mpaka Mwenyezi Mungu ahukumu, na Yeye ndiye mbora wa wanaohukumu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wewe fuata yanayo funuliwa kwako kwa wahyi. Na vumilia mpaka Mwenyezi Mungu ahukumu, na Yeye ndiye mbora wa mahakimu. [109]

[109] Ewe Mtume! Thibiti juu ya Dini ya Haki. Na fuata wahyi ulio teremshiwa, nawe uwe na subira kwa maudhi yanayo kufika kwa ajili ya Njia ya Da'wa (Wito), mpaka Mwenyezi Mungu ahukumu baina yako na wao, kwa vile alivyo kuahidi kuwa atawapa ushindi Waumini, na watahizika makafiri. Na Yeye ndiye mbora wa mahakimu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na uufuate, ewe Mtume, wahyi wa Allah Mtukufu Aliokutumia wewe na uutumie kivitendo. Na uwe na subira katika kumtii Allah Mtukufu, Aliyetukuka, na katika kujiepusha na mambo ya kumuasi na kwa kuvumilia makero ya wenye kukukera katika kuufikisha ujumbe Wake, mpaka Allah Mtukufu Atoe uamuzi Wake kwao na kwako. Na Yeye, Aliyetukuka na kuwa juu, Ndiye mbora wa kutoa uamuzi, kwa kuwa uamuzi Wake unakusanya uadilifu uliokamilika.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yunus

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net