Yunus 10:108
يونسقُلْ يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ قَدْ جَآءَكُمُ ٱلْحَقُّ مِن رَّبِّكُمْ ۖ فَمَنِ ٱهْتَدَىٰ فَإِنَّمَا يَهْتَدِى لِنَفْسِهِۦ ۖ وَمَن ضَلَّ فَإِنَّمَا يَضِلُّ عَلَيْهَا ۖ وَمَآ أَنَا۠ عَلَيْكُم بِوَكِيلٍ
Sema: Enyi watu! Haki imekwishawajia kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Kwa hivyo, anayeongoka, basi anaongoka kwa faida ya nafsi yake, na anayepotea, basi anapotea kwa hasara ya nafsi yake. Na mimi si mwakilishi juu yenu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Sema: Enyi watu! Haki imekwisha kukujieni kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Basi anaye ongoka anaongoka kwa faida ya nafsi yake, na anaye potea anapotea kwa khasara ya nafsi yake. Na mimi si mwakilishi juu yenu. [108]
[108] Ewe Mtume! Fikisha wito wa Mwenyezi Mungu kwa watu wote! Na waambie: Enyi watu! Hakika Mwenyezi Mungu amekuteremshieni Sharia ya Haki kutokana naye. Anaye taka kuongoka basi afanye haraka. Kwani faida ya uwongofu wake utamrejea mwenyewe. Na mwenye kushikilia upotovu utamuangukia mwenyewe. Na mimi sikuwakilishwa nikulazimisheni muamini, wala kukutawalini.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Sema, ewe Mtume, kuwaambia hawa watu, «Amewajia nyinyi Mtume wa Allah Mtukufu na Qur’ani ambayo ndani yake muna maelezo ya kuwaongoa nyinyi. Basi mwenye kuongoka kwa uongofu wa Allah Mtukufu, hakika matunda ya kitendo chake yatamrudia yeye mwenyewe. Na mwenye kupotoka akawa kando na haki na akaendelea kwenye upotevu, hakika upotevu wake na madhara yake yatamshukia yeye mwenyewe. Na mimi si kuwakilishwa kwenu mpaka muwe Waumini. Mimi ni mjumbe mwenye kufikisha, nawafikishia yale niliyotumwa kwayo».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net