Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 10 · Aya ya 107

Yunus 10:107

يونس

وَإِن يَمْسَسْكَ ٱللَّهُ بِضُرٍّ فَلَا كَاشِفَ لَهُۥٓ إِلَّا هُوَ ۖ وَإِن يُرِدْكَ بِخَيْرٍ فَلَا رَآدَّ لِفَضْلِهِۦ ۚ يُصِيبُ بِهِۦ مَن يَشَآءُ مِنْ عِبَادِهِۦ ۚ وَهُوَ ٱلْغَفُورُ ٱلرَّحِيمُ

Maana

Na Mwenyezi Mungu akikugusa kwa madhara, basi hakuna wa kukuondolea isipokuwa Yeye. Na akikutakia heri, basi hakuna wa kurudisha fadhila yake. Humsibu kwayo amtakaye katika waja wake, na Yeye ndiye Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na Mwenyezi Mungu akikugusisha madhara, basi hapana wa kukuondolea ila Yeye. Na akikutakia kheri, basi hapana awezaye kurudisha fadhila yake.Huifikisha kwa amtakaye katika waja wake, na Yeye ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu. [107]

[107] Ewe Nabii! Yakikusibu madhara kutoka kwa Mwenyezi Mungu, hapana wa kuyaondoa ila Yeye. Na akikujaalia kheri hapana anaye weza kukunyima yeyote. Kwani yeye anagawa kheri kuwapa waja wake kwa fadhila yake. Na Yeye Subhanahu ni Mkunjufu wa maghfira, Mkuu wa rehema.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na Allah Mtukufu Akikupatia, ewe Mtume, shida au mitihani, basi hakuna wa kuyaondoa hayo isipokuwa Yeye, Aliyetukuka na kuwa juu, na Akikutakia furaha na neema, basi hakuna yoyote mwenye kuyazuia hayo. Allah Mtukufu, Aliyetukuka na kuwa juu, Anampatia furaha na shida Anayemtaka kati ya waja Wake. Na Yeye ni Mwingi wa msamaha wa dhambi za wenye kutubia, ni Mwingi wa rehema kwa wanaomuamini na kumtii.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yunus

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net