Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 10 · Aya ya 106

Yunus 10:106

يونس

وَلَا تَدْعُ مِن دُونِ ٱللَّهِ مَا لَا يَنفَعُكَ وَلَا يَضُرُّكَ ۖ فَإِن فَعَلْتَ فَإِنَّكَ إِذًا مِّنَ ٱلظَّـٰلِمِينَ

Maana

Na wala usiombe badala ya Mwenyezi Mungu wale ambao hawakufai kitu wala hawakudhuru. Na ukifanya hivyo, basi wewe hakika ni miongoni mwa madhalimu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wala usiwaombe wasio kuwa Mwenyezi Mungu ambao hawakufai kitu wala hawakudhuru. Ukifanya hivyo basi utakuwa miongoni mwa walio dhulumu. [106]

[106] Wala usimkimbilie kwa kumwomba na kumuabudu yeyote asiye kuwa Mwenyezi Mungu. Hao hawakuletei manufaa wala madhara. Ukifanya hayo inakuwa umekwisha ingia miongoni mwa washirikina walio dhulumu. Na anayo katazwa Nabii, ndio wanakatazwa umma wake wote. Na hivyo ndio ukomo wa kukanya. Kwani kumkanya ambaye hayumkiniki kutenda anacho kanywa, ndio hadi ya kukanya.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Wala usiwaombe, ewe Mtume, wasiokuwa Allah Mtukufu miongoni mwa mizimu na masanamu, kwani wao hawanufaishi wala hawadhuru. Na ufanyapo hilo na ukawaomba wasiokuwa Allah Mtukufu, hapo wewe utakuwa ni miongoni mwa wenye kumshirikisha Allah Mtukufu, wenye kujidhulumu nafsi zao kwa ushirikina na kufanya maasia. Maneno haya ingawa anaambiwa Mtume, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), pia wanaambiwa ummah wote.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yunus

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net