Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 10 · Aya ya 105

Yunus 10:105

يونس

وَأَنْ أَقِمْ وَجْهَكَ لِلدِّينِ حَنِيفًا وَلَا تَكُونَنَّ مِنَ ٱلْمُشْرِكِينَ

Maana

Na kwamba uuelekeze uso wako kwenye Dini ya kweli, kwa unyofu wala kamwe usiwe katika washirikina.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na uelekeze uso wako kwenye Dini ya Kweli, wala usiwe katika washirikina. [105]

[105] Ewe Nabii! Simama sawasawa, umuelekee Mwenyezi Mungu vilivyo. Wala usijitie katika miongoni mwa walio mshirikisha Mwenyezi Mungu. Epukana nao, na uwe mbali nao, wewe na Waumini wanao kufuata.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na ujisimamishe imara, ewe Mtume, juu ya dini ya Uislamu, hali ya kulingana sawa juu yake, usiwe ni mwenye kupotoka na kuwa kando nayo ukaelekea kwenye Uyahudi au Unaswara wala kumuabudu asiyekuwa Yeye. Wala usiwe ni miongoni mwa wale wanaoshirikisha, katika ibada ya Mola wao, waungu na wale wanaodai kuwa wanafanana na Yeye, kwani ufanyapo hilo utakuwa ni miongoni mwa watakaoangamia. Maneno haya ingawa anaambiwa Mtume, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), pia wanaambiwa ummah wote.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yunus

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net