Al-Faatiha 1:6
الفاتحةٱهْدِنَا ٱلصِّرَٰطَ ٱلْمُسْتَقِيمَ
Tuongoe kwenye njia iliyonyooka.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Tuongoe njia iliyonyooka. [6]
[6] Tunakuomba utuwafikishe kuendea Njia ya haki, na kheri na mafanikio.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Tuonyeshe, tuongoze na tupe taufiki ya kuelekea njia iliyonyoka na ututhibitishe juu yake mpaka tukutane na wewe, nayo ni Uislamu ambao ndio njia iliyo wazi yenye kufikisha kwenye radhi za Allah Mtukufu na kwenye Pepo yake, njia tuliyoonyeshwa na aliye mwisho wa Mitume wa Allah Mtukufu na Manabii Wake, Muhammad, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie, kwani hakuna kufaulu kwa mja isipokuwa kwa kusimama imara juu yake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net