Al-Faatiha 1:5
الفاتحةإِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ
Ni Wewe tu tunayeabudu, na ni Wewe tu tunayeomba msaada.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wewe tu tunakuabudu, na wewe tu tunakuomba msaada. [5]
[5] Hatumuabudu yeyote ila Wewe tu, wala hatutaki msaada kwa yeyote ila kwako tu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Sisi tunakuabudu wewe peke yako, na tunataka msaada kwako peke yako katika mambo yetu yote. Mambo yote yako mkononi mwako, hakuna asiyekuwa wewe anayemiliki chochote katika hayo hata kadiri ya uzito wa chungu mdogo. Katika aya hii kuna dalili ya kuwa mja haifai aelekeze kitu chochote miongoni mwa aina za ibada, kama kuomba, kutaka kunusuriwa, kuchinja na kutufu, isipokuwa kwa Allah Mtukufu Peke Yake. Pia ndani yake kuna ponya ya nyoyo kutokana na ugonjwa wa kufungamana na asiyekuwa Allah Mtukufu, na kutokana na ugonjwa wa ria, kujiona na kiburi.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net