Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Kuamini Malaika

Hadithi 7

Dua ya mtu muislamu kwa ndugu yake, anapokuwa hayupo, hujibiwa

عَن أُمِّ الدَّرْدَاءِ وَ أَبِي الدَّرداءِ رَضيَ اللهُ عنهما أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَانَ يَقُولُ: «دَعْوَةُ الْمَرْءِ الْمُسْلِمِ لِأَخِيهِ بِظَهْرِ الْغَيْبِ مُسْتَجَابَةٌ، عِنْدَ رَأْسِهِ مَلَكٌ مُوَكَّلٌ كُلَّمَا دَعَا لِأَخِيهِ بِخَيْرٍ، قَالَ الْمَلَكُ الْمُوَكَّلُ بِهِ: آمِينَ وَلَكَ بِمِثْلٍ».
Kutoka kwa Ummu Dardaai na Abuu Dardaai radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao, ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa akisema: "Dua ya mtu muislamu kwa ndugu yake, anapokuwa hayupo, hujibiwa, kichwani kwake huwa kuna Malaika aliyepewa kazi, kila anapomuombea ndugu yake kwa heri, Malaika aliyepewa kazi hiyo husema: Ewe Mwenyezi Mungu pokea dua, na kwako pia upate mfano wake".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa dua ya muislamu kwa ndugu yake muislamu, anapokuwa hayupo anayeombewa dua, hujibiwa; kwa sababu huwa na kiwango kikubwa cha utakasifu (Ikhlaswi) na kwamba kichwani kwa muombaji huwa kuna Malaika aliwakilishwa, kila anapomuombea ndugu yake kwa heri, basi anasema Malaika alipewa kazi hiyo: Mwenyezi Mungu apokee dua, na upate pia mfano wa hayo uliyoomba.

Mafunzo
  1. Himizo kwa waumini la kutendeana wema wao kwa wao walau hata kwa dua.
  2. Dua ya siri inaonyesha dalili wazi juu ya imani ya kweli na udugu.
  3. Kufungamanishwa dua na siri; ni kwa sababu hilo huwa katika kiwango kikubwa cha utakasifu, na kuhudhuria moyo.
  4. Miongoni mwa sababu za kujibiwa dua ni mtu kumuombea ndugu yake kwa siri.
  5. Amesema Nawawi: Fadhila ya dua kwa ndugu yake muislamu kwa siri, na hata akiwaombea watu wengi katika waislamu pia atapata fadhili hii, na hata akiwaombea waislamu wote kwa ujumla, pia inavyoonekana atapata fadhila hizi, na walikuwa baadhi ya wema waliotangulia anapotaka kujiombea mwenyewe basi anamuombea ndugu yake muislamu dua hiyo; kwa sababu inajibiwa, na yeye anapata mfano wake.
  6. Hapa kumebainishwa baadhi ya kazi za Malaika, na kwamba wako miongoni mwao aliowapa Mwenyezi Mungu kazi hii.
Marejeo

صحيح مسلم (4/ 2094) (2733). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 585). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (2/ 1018). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (6/ 48). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (17/ 510).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Hakika mmoja wenu hukusanywa umbile lake ndani ya tumbo la mama yake siku arobaini

عَنْ أَبِي عَبْدِ الرَّحْمَنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ مَسْعُودٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: حَدَّثَنَا رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَهُوَ الصَّادِقُ المَصْدُوقُ: «إِنَّ أَحَدَكُمْ يُجْمَعُ خَلْقُهُ فِي بَطْنِ أُمِّهِ أَرْبَعِينَ يَوْمًا، ثُمَّ يَكُونُ عَلَقَةً مِثْلَ ذَلِكَ، ثُمَّ يَكُونُ مُضْغَةً مِثْلَ ذَلِكَ، ثُمَّ يُرْسَلُ إلَيْهِ المَلَكُ فَيَنْفُخُ فِيهِ الرُّوحَ، وَيُؤْمَرُ بِأَرْبَعِ كَلِمَاتٍ: بِكَتْبِ رِزْقِهِ، وَأَجَلِهِ، وَعَمَلِهِ، وَشَقِيٍّ أَوْ سَعِيدٍ؛ فَوَالَّذِي لَا إلَهَ غَيْرُهُ إنَّ أَحَدَكُمْ لَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أَهْلِ الجَنَّةِ حَتَّى مَا يَكُونُ بَيْنَهُ وَبَيْنَهَا إلَّا ذِرَاعٌ فَيَسْبِقُ عَلَيْهِ الكِتَابُ فَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أَهْلِ النَّارِ فَيَدْخُلُهَا، وَإِنَّ أَحَدَكُمْ لَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أَهْلِ النَّارِ حَتَّى مَا يَكُونُ بَيْنَهُ وَبَيْنَهَا إلَّا ذِرَاعٌ، فَيَسْبِقُ عَلَيْهِ الكِتَابُ فَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أَهْلِ الجَنَّةِ فَيَدْخُلُهَا».
Imepokewa kutoka kwa Abuu Abdirahman Abdullahi Bin Masoud radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Alituhadithia Mtume rehema na amani ziwe juu yake naye ndiye mkweli mwenye kusadikika: "Hakika mmoja wenu hukusanywa umbile lake ndani ya tumbo la mama yake siku arobaini, kisha linakuwa pande la damu kwa mfano wake, kisha linakuwa pande la nyama mfano wake (siku arobaini), kisha linatumiwa Malaika analipulizia roho, na anaamrishwa kuandika maneno manne: Kuandika riziki yake, na umri wake, na matendo yake, na kuwa ni muovu au mwema; namuapa yule ambaye hakuna Mola isipokuwa yeye hakika mmoja wenu atafanya amali za watu wa Peponi mpaka ikawa baina yake na Peponi ni dhiraa moja (futi) kikamtangulia kitabu akafanya amali za watu wa motoni akauingia, na hakika mmoja wenu atafanya amali za watu wa motoni mpaka ikawa baina yake na Moto isipokuwa dhiraa, kitabu kikamtangulia akafanya amali za watu wa Peponi na akaingia".
Imepokelewa na Bukhari na MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Amesema Bin Masoud: Ametuhadithia Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake naye ni mkweli kwenye maneno yake, na mwenye kukubaliwa, Mwenyezi Mungu Mtukufu amemkubali, Amesema: Kwa hakika mmoja wenu hukusanywa umbile lake, na jambo hilo ni kuwa mtu akimuingilia mke wake basi yale manii yake yaliyosambaa hukusanywa kwenye tumbo la mwanamke kwa muda wa siku arobaini yakiwa ni tone la manii, Kisha hubadilika na kuwa pande la damu nzito iliyoganda, haya hufanyika katika arobaini ya pili, Kisha hubadilika kuwa pande la nyama, nacho ni kipande cha nyama chenye ukubwa wa kuweza kutafunwa, na mabadiliko haya ni katika arobaini ya tatu, Kisha Mwenyezi Mungu hulitumia pande hilo la nyama Malaika, kisha hulipulizia ndani yake roho baada ya kuisha siku arobaini za tatu, Na huamrishwa Malaika aandike maneno manne, nayo ni: Riziki yake, nacho ni kiwango ambacho atakipata miongoni mwake ni neema katika umri wake, Na pia huandikwa wakati wake, nao ni muda wa kubakia kwake Duniani, Na matendo yake, yatakuwa ni yapi? Na je atakuwa muovu au mwema. Kisha akaapa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa yawezekana mtu akafanya matendo miongoni mwa matendo ya watu wa peponi, na yakawa matendo yake ni mazuri, yaani kwenye muonekano wa watu, na akabakia hivyo mpaka inakuwa kati yake na Pepo ni kiasi cha mkono, yaani kiasi kilichobaki kati yake mpaka kuifikia pepo ni kidogo sana kama vile ambavyo mtu amebakiza nafasi kati yake na ardhi kiasi cha mkono, mara Kitabu kinamtangulia na kile alichopangiwa, na wakati huo anafanya matendo ya watu wa motoni na akaandikiwa kuwa huo ndio mwisho wake na akaingia motoni; Kwa sababu sharti la kukubaliwa matendo yake ni kudumu katika matendo hayo na wala asibadilishe, na watu wengine wapo wenye kufanya matendo ya watu wa motoni mpaka mtu anakaribia kuingia motoni, mpaka inakuwa kati yake na kuingia motoni ni kiasi cha urefu wa mkono, basi kikamtangulia kitabu na alichopangiwa hivyo akafanya matendo ya watu wa peponi na akaingia peponi.

Mafunzo
  1. Kumebainishwa hatua za uumbwaji wa mwanadamu.
  2. Kuamini hukumu na kadari.
  3. Mwisho wa mambo yote huwa kwa namna ambavyo imekwishapangwa na kukadiriwa.
  4. Tahadhari ya kutodanganyika na muonekano wa matendo; Bali matendo huangaliwa mwisho wake.
Marejeo

صحيح البخاري (9/ 135) (7454)، (4/ 111) (3208). صحيح مسلم (4/ 2036) (2643). عمدة القاري شرح صحيح البخاري (15/ 130). شرح الأربعين النووية للعثيمين (ص: 84).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com