عن ابن عباس رضي الله عنهما قال: جاءَ رجُلُ إلى النبي صلى الله عليه وسلم فقال: يا رسولَ اللهِ، إن أحدنا يجدُ في نفسِهِ -يُعرِّضُ بالشَّيءِ- لأَن يكونَ حُمَمَةً أحَبُّ إليه من أن يتكلَّم بِهِ، فقال: «اللهُ أكبرُ، اللهُ أكبرُ، الحمدُ لله الذي ردَّ كيدَه إلى الوسوسَةِ».
Imepokelewa kutoka kwa Bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na baba yake amesema: Alikuja mtu mmoja kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, hakika mmoja wetu anatokewa na jambo kwenye nafsi yake kiasi yakuwa anaona bora akachomwa mpaka akawa jivu ni bora kwake kuliko kulizungumza jambo hilo, akasema: "Allahu Akbar, Allahu Akbar Mwenyezi Mungu ni mkubwa Mwenyezi Mungu ni mkubwa, namshukuru Mwenyezi Mungu ambaye amevirudisha vitimbi vya Shetani na vikageuka kuwa ni wasiwasi".
Imepokelewa na Abu Daud na Nasai katika AlkubraaDarajaSahihi
Maelezo
Alikuja mtu mmoja kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, mmoja wetu hutokewa na jambo kwenye nafsi yake kiasi yakuwa anaona bora akachomwa mpaka akawa jivu ni bora kwake kuliko kulizungumza jambo hilo. Basi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akapiga Takbira mara mbili na akamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kurudisha vitimbi vya shetani na kuvigeuza kuwa ni wasiwasi,
Mafunzo
- Kumewekwa wazi kuwa Shetani humuwinda muislamu kwa njia ya wasiwasi; ili kumtoa katika imani na kumuingiza katika ukafiri.
- Kumewekwa wazi kuwa shetani ni kiumbe dhaifu mbele ya wenye imani, kwani Shetani hawezi kufanya chochote zaidi ya kutia wasiwasi.
- Muumini anapasa kuupinga wasiwasi utokanao na shetani na kuuzuia wasiwasi huo.
- Ni sheria kuleta Takbira kwenye jambo zuri au lenye kufanana na mambo mazuri.
- Ni katika sheria muislamu kumuuliza mtu mjuzi kwa kila jambo linalomtatiza.
Marejeo
سنن أبي داود (7/ 435) (5112) السنن الكبرى للنسائي (9/ 249) (10435)، شرح سنن أبي داود للعباد (580/ 28)، صحيح مسلم (1/ 119) (132)، شرح سنن أبي داود لابن رسلان (19/370)، ومرقاة الصعود (3/1301).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعن عُثْمَانَ بْنَ أَبِي الْعَاصِ رضي الله عنه: أنه أَتَى النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَالَ: يَا رَسُولَ اللهِ، إِنَّ الشَّيْطَانَ قَدْ حَالَ بَيْنِي وَبَيْنَ صَلَاتِي وَقِرَاءَتِي يَلْبِسُهَا عَلَيَّ، فَقَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «ذَاكَ شَيْطَانٌ يُقَالُ لَهُ خِنْزَِبٌ، فَإِذَا أَحْسَسْتَهُ فَتَعَوَّذْ بِاللهِ مِنْهُ، وَاتْفُلْ عَلَى يَسَارِكَ ثَلَاثًا»، قَالَ: فَفَعَلْتُ ذَلِكَ فَأَذْهَبَهُ اللهُ عَنِّي.
Kutoka kwa Othman bin Abil Aswi -Radhi za Allah ziwe juu yake-: Yakwamba yeye alimwendea Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hakika shetani amekaa kati yangu na swala yangu na kisomo changu ananichanganya, akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Huyo ni Shetani anaitwa Khinzab, ukimuhisi basi haraka sana taka ulinzi kutoka kwa Allah dhidi yake, na uteme kushotoni kwako mara tatu", anasema: Nikafanya hivyo Mwenyezi Mungu akamuondosha kwangu.
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Alikuja Othman bin Abil Aswi -Radhi za Allah ziwe juu yake- kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu hakika Shetani ameziba kati yangu na swala yangu, na amenizuilia na kupata utulivu ndani yake, na amenichanganyia kisomo changu na amenitia wasi wasi ndani yake, Akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Huyo ni Shetani aitwaye Khinzab, ukihisi hali hii basi taka kinga kwa Allah, na utake ulinzi kutoka kwa Allah dhidi yake, na uteme mate kushotoni kwako mara tatu, Othman anasema: Nikafanya aliyoniamrisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Mwenyezi Mungu akaniondolea hali hiyo.
Mafunzo
- Umuhimu wa utulivu na kuhudhurisha moyo ndani ya sala, na kuwa Shetani anajitahidi kutia tashiwishi na shaka ndani yake.
- Sunna ya kutaka ulinzi kutokana na shetani wakati wa wasi wasi wake ndani ya sala, pamoja na kutema kushoto mara tatu.
- Kumebainishwa waliyokuwa nayo Masahaba -Radhi za Allah ziwe juu yao- katika swala la kurudi kwao kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- katika yale yanayojitokeza kwao miongoni mwa changamoto ili azitatue.
- Maisha ya nyoyo za Masahaba, na kwamba hima yao kubwa ilikuwa ni Akhera.
Marejeo
صحيح مسلم (4/ 1728) (2203)، إكمال المعلم (7/110)، شرح النّووي على مسلم (14/190)، البحر المحيط الثجاج في شرح صحيح الإمام مسلم بن الحجاج (36/ 136).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com