Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa dua ya muislamu kwa ndugu yake muislamu, anapokuwa hayupo anayeombewa dua, hujibiwa; kwa sababu huwa na kiwango kikubwa cha utakasifu (Ikhlaswi) na kwamba kichwani kwa muombaji huwa kuna Malaika aliwakilishwa, kila anapomuombea ndugu yake kwa heri, basi anasema Malaika alipewa kazi hiyo: Mwenyezi Mungu apokee dua, na upate pia mfano wa hayo uliyoomba.
- Himizo kwa waumini la kutendeana wema wao kwa wao walau hata kwa dua.
- Dua ya siri inaonyesha dalili wazi juu ya imani ya kweli na udugu.
- Kufungamanishwa dua na siri; ni kwa sababu hilo huwa katika kiwango kikubwa cha utakasifu, na kuhudhuria moyo.
- Miongoni mwa sababu za kujibiwa dua ni mtu kumuombea ndugu yake kwa siri.
- Amesema Nawawi: Fadhila ya dua kwa ndugu yake muislamu kwa siri, na hata akiwaombea watu wengi katika waislamu pia atapata fadhili hii, na hata akiwaombea waislamu wote kwa ujumla, pia inavyoonekana atapata fadhila hizi, na walikuwa baadhi ya wema waliotangulia anapotaka kujiombea mwenyewe basi anamuombea ndugu yake muislamu dua hiyo; kwa sababu inajibiwa, na yeye anapata mfano wake.
- Hapa kumebainishwa baadhi ya kazi za Malaika, na kwamba wako miongoni mwao aliowapa Mwenyezi Mungu kazi hii.
صحيح مسلم (4/ 2094) (2733). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 585). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (2/ 1018). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (6/ 48). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (17/ 510).