Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

“Mwenye kupigana ili neno la Mwenyezi Mungu liwe juu, basi huyo yuko katika Njia ya Mwenyezi Mungu

عَنْ أَبِي مُوسَى رضي الله عنه قَالَ: سُئِلَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنِ الرَّجُلِ يُقَاتِلُ شَجَاعَةً، وَيُقَاتِلُ حَمِيَّةً، وَيُقَاتِلُ رِيَاءً، أَيُّ ذَلِكَ فِي سَبِيلِ اللهِ؟ فَقَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «مَنْ قَاتَلَ لِتَكُونَ كَلِمَةُ اللهِ هِيَ الْعُلْيَا، فَهُوَ فِي سَبِيلِ اللهِ».
Kutoka kwa Abuu Musa Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Aliulizwa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake kuhusu mtu anayepigana kwa kutaka kuonekana jasiri, na anayepigana kwa hamasa za ukabila, au anayepigana kwa kutaka kuonekana. Ni yupi kati ya hao anayepigana kwa ajili ya Mwenyezi Mungu? Akasema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake: “Mwenye kupigana ili neno la Mwenyezi Mungu liwe juu, basi huyo yuko katika Njia ya Mwenyezi Mungu."
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliulizwa kuhusu kutofautiana kwa malengo ya wapiganaji hao; mwenye kupigana kwa kutaka kuonekana jasiri, au kwa hamasa, au ionekane nafasi yake kati ya watu, au mengineyo, ni lipi kati ya haya lipo kwa ajili ya Allah? Akaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa mpiganaji katika njia ya Mwenyezi Mungu ni yule anayepigana ili neno la Mwenyezi Mungu liwe juu.

Mafunzo
  1. Msingi katika kutengemaa kwa matendo na kuharibika kwake ni nia na kutakasa matendo kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.
  2. Ikiwa lengo la Jihadi ni kulinyanyua neno la Mwenyezi Mungu, na likaunganishwa na lengo lingine la kisheria, kama vile kupata ngawira, basi haidhuru nia yake ya asili.
  3. Kuwazuia maadui dhidi ya nchi na kulinda heshima za watu ni katika kupigana kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.
  4. Fadhila ziliyotajwa kwa wapiganaji zinawahusu wale waliopigana ili neno la Mwenyezi Mungu liwe kuu.
Marejeo

صحيح البخاري (9/ 136) (7458). صحيح مسلم (3/ 1513) (1904). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، لعبد الله البسام (ص753). الإعلام بفوائد عمدة الأحكام، لابن الملقن (10/ 380).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Adabu za Jihadi.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com