عَنِ ابْنِ عُمَرَ رَضيَ اللهُ عنهما قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «إِذَا جَمَعَ اللهُ الْأَوَّلِينَ وَالْآخِرِينَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ يُرْفَعُ لِكُلِّ غَادِرٍ لِوَاءٌ، فَقِيلَ: هَذِهِ غَدْرَةُ فُلَانِ بْنِ فُلَانٍ».
Kutoka kwa bin Omari radhi za Allah ziwe juu yao yeye na baba yake, amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake: "Pindi atakapaowakusanya Mwenyezi Mungu wa mwanzo na wa mwisho siku ya Kiyama itanyanyuliwa bendera kwa kila haini, patasemwa: Hii ndio hiana ya fulani bin fulani".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu siku ya Kiyama atakapowakusanya wa mwanzo na wa mwisho kwa ajili ya hesabu, atasimika kwa kila haini ambaye hakutimiza ahadi aliyokubaliana nayo kwa Mwenyezi Mungu au pamoja na watu, alama ambayo atamfedhehesha kwayo mbele za watu kwa sababu ya hiana yake, na kutanadiwa juu yake siku hiyo: Hii ndio hiana ya fulani bin fulani; kwa ajili ya kutangaza ubaya wa kitendo chake mbele ya waliokusanyika katika uwanja halaiki (mahashari).
Mafunzo
- Uharamu wa hiana na kwamba hilo ni katika madhambi makubwa; kwa sababu ndani yake kuna ahadi hii kali ya adhabu.
- Hiana iliyosemwa katika hadithi inakusanya kila aliyekuamini juu ya damu, au heshima, au siri, au mali, kisha ukamfanyia hiana, na ukaenda kinyume na dhana yake katika kukuamini kwake.
- Amesema Qurtubi: Hili ni tamko kutoka kwake linawahusu waarabu kwa sababu ya yale waliyokuwa wakiyafanya; kwani wao walikuwa wakinyanyua bendera nyeupe kwa ajili ya kutimiza ahadi, na kwa usaliti bendera nyeusi, ili wamlaumu haini na wamkemee, hadithi ikapelekea kutokea mfano wa hilo kwa haini; ili awe mashuhuri kwa sifa yake hiyo siku ya Kiyama, na watamsema kwa ubaya waliosimama katika uwanja huo.
- Amesema bin Hajari: Na katika hadithi hii nikuwa watu siku ya Kiyama wataitwa kwa ubini wa baba zao; kwa kauli yake aliposema: "Huu ni usaliti wa fulani bin fulani".
Marejeo
صحيح البخاري (4/ 104) (3188)
صحيح مسلم (3/ 1359) (1735).
تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، للبسام (ص745).
الإلمام بشرح عمدة الأحكام، لإسماعيل الأنصاري (2/ 188).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ عَبْدِ اللَّهِ بنِ عُمَرَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُما: أَنَّ امْرَأَةً وُجِدَتْ فِي بَعْضِ مَغَازِي النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مَقْتُولَةً، فَأَنْكَرَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَتْلَ النِّسَاءِ وَالصِّبْيَانِ.
Imepokelewa kutoka kwa Abdallah bin Omari -Radhi za Allah ziwe juu yake na baba yake-: Ya kwamba mwanamke mmoja alipatikana akiwa kauwawa katika moja ya vita vya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akakemea vikali Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuuwawa wanawake na watoto.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliona mwanamke akiwa kauwawa katika moja ya vita, akakemea vikali kuuwawa wanawake na watoto ambao hawajafikia balehe.
Mafunzo
- Mwanamke na mtoto yeyote ambaye hatopigana, na mwenyekuwa mfano wao kama wazee vikongwe, na watawa, hawa hawauawi, madam hawajatoa rai au msaada wowote wa kuwapiga waislamu, ikiwa watafanya hivyo basi nao watauawa.
- Katazo la kuwaua wanawake na watoto; kwa sababu hawa huwa hawawapigi vita waislamu, na malengo ya kupigana katika njia ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, ni kuvunja nguvu ya wapiganaji pekee, ili ujumbe wa haki uwafikie watu wote.
- Huruma ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake mpaka katika mapambano na vita.
Marejeo
صحيح البخاري (4/ 61) (3014).
صحيح مسلم (3/ 1364) (1744).
الإلمام بشرح عمدة الأحكام، لإسماعيل الأنصاري (2/ 189).
تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، للبسام (ص746).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ أَبِي مُوسَى رضي الله عنه قَالَ: سُئِلَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنِ الرَّجُلِ يُقَاتِلُ شَجَاعَةً، وَيُقَاتِلُ حَمِيَّةً، وَيُقَاتِلُ رِيَاءً، أَيُّ ذَلِكَ فِي سَبِيلِ اللهِ؟ فَقَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «مَنْ قَاتَلَ لِتَكُونَ كَلِمَةُ اللهِ هِيَ الْعُلْيَا، فَهُوَ فِي سَبِيلِ اللهِ».
Kutoka kwa Abuu Musa Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Aliulizwa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake kuhusu mtu anayepigana kwa kutaka kuonekana jasiri, na anayepigana kwa hamasa za ukabila, au anayepigana kwa kutaka kuonekana. Ni yupi kati ya hao anayepigana kwa ajili ya Mwenyezi Mungu? Akasema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake: “Mwenye kupigana ili neno la Mwenyezi Mungu liwe juu, basi huyo yuko katika Njia ya Mwenyezi Mungu."
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliulizwa kuhusu kutofautiana kwa malengo ya wapiganaji hao; mwenye kupigana kwa kutaka kuonekana jasiri, au kwa hamasa, au ionekane nafasi yake kati ya watu, au mengineyo, ni lipi kati ya haya lipo kwa ajili ya Allah? Akaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa mpiganaji katika njia ya Mwenyezi Mungu ni yule anayepigana ili neno la Mwenyezi Mungu liwe juu.
Mafunzo
- Msingi katika kutengemaa kwa matendo na kuharibika kwake ni nia na kutakasa matendo kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.
- Ikiwa lengo la Jihadi ni kulinyanyua neno la Mwenyezi Mungu, na likaunganishwa na lengo lingine la kisheria, kama vile kupata ngawira, basi haidhuru nia yake ya asili.
- Kuwazuia maadui dhidi ya nchi na kulinda heshima za watu ni katika kupigana kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.
- Fadhila ziliyotajwa kwa wapiganaji zinawahusu wale waliopigana ili neno la Mwenyezi Mungu liwe kuu.
Marejeo
صحيح البخاري (9/ 136) (7458).
صحيح مسلم (3/ 1513) (1904).
تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، لعبد الله البسام (ص753).
الإعلام بفوائد عمدة الأحكام، لابن الملقن (10/ 380).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعنْ ابنِ مَسْعُودٍ رَضيَ اللهُ عنهُ قَالَ: كُنَّا مَعَ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي سَفَرٍ، فَانْطَلَقَ لِحَاجَتِهِ، فَرَأَيْنَا حُمَّرَةً مَعَهَا فَرْخَانِ، فَأَخَذْنَا فَرْخَيْهَا، فَجَاءَتِ الْحُمَرَةُ فَجَعَلَتْ تَفْرِشُ، فَجَاءَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَالَ: «مَنْ فَجَعَ هَذِهِ بِوَلَدِهَا؟ رُدُّوا وَلَدَهَا إِلَيْهَا»، وَرَأَى قَرْيَةَ نَمْلٍ قَدْ حَرَّقْنَاهَا، فَقَالَ: «مَنْ حَرَّقَ هَذِهِ؟» قُلْنَا: نَحْنُ. قَالَ: «إِنَّهُ لَا يَنْبَغِي أَنْ يُعَذِّبَ بِالنَّارِ إِلَّا رَبُّ النَّارِ».
Kutoka kwa bin Masoud radhi za Allahi ziwe juu yake amesema: Tulikuwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika safari, akaondoka kwa ajili ya haja yake, tukaona ndege akiwa na makinda mawili, tukawachukua makinda wake, akaja yule ndege akaanza kupepesa mbawa zake, basi akaja Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema: "Ni nani aliyemuhuzunisha ndege huyu kwa mwanaye? Mrejesheeni mwanaye", na akaona kijiji cha wadudu chungu tulichokichoma kwa moto, akasema: "Hakika hastahiki kuadhibu kwa Moto isipokuwa Mola Mlezi wa Moto".
Imepokelewa na Abu DaudDarajaSahihi
Maelezo
Ameeleza Abdallah bin Masudi radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake ya kwamba wao walikuwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika safari, akaondoka rehema na amani ziwe juu yake kwa ajili kukidhi haja yake, Maswahaba zake wakapata ndege aina ya Hummara akiwa na makinda mawili, wakayachukua, yule ndege akaanza kupeperusha mbawa zake na kuzipepesa kwa huzuni kwa kuwakosa makinda wake, akaja rehema na amani ziwe juu yake na akasema: Ni nani aliyemuhuzunisha na akamuhofisha kwa kuchukua vitoto vyake? Kisha akaamrisha virejeshwe kwake. Kisha akaona kijiji cha wadudu chungu kilichochomwa kwa moto, akasema rehema na amani ziwe juu yake: Ni nani aliyekiunguza hiki? Wakasema baadhi ya Maswahaba: Sisi. Akasema kuwaambia: Hakika haifai kwa yeyote kuadhibu kiumbe hai kwa moto; isipokuwa Mwenyezi Mungu muumba wake.
Mafunzo
- Sheria ya kujisitiri kwa ajili ya kukidhi haja.
- Katazo la kuwaadhibu wanyama kwa kuchukua watoto wao.
- Katazo la kuwachoma sisimizi na wadudu wengineo kwa moto.
- Himizo la upole na huruma kwa wanyama, na Uislamu ndio ulitangulia kulisema hilo.
- Huruma yake rehema na amani ziwe juu yake kwa wanyama.
- Kuadhibu kwa moto ni miongoni mwa mambo anayohusika nayo Mola Mtukufu pekee.
Marejeo
سنن أبي داود (4/ 309) (2675).
نزهة المتقين، لمجموعة من الباحثين (2/ 1105).
كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (19/ 150).
بهجة الناظرين، لسليم الهلالي (3/ 120).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (6/ 300).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comKila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com