Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Ya kwamba mwanamke mmoja alipatikana akiwa kauwawa katika moja ya vita vya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akakemea vikali Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuuwawa wanawake na watoto

عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بنِ عُمَرَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُما: أَنَّ امْرَأَةً وُجِدَتْ فِي بَعْضِ مَغَازِي النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مَقْتُولَةً، فَأَنْكَرَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَتْلَ النِّسَاءِ وَالصِّبْيَانِ.
Imepokelewa kutoka kwa Abdallah bin Omari -Radhi za Allah ziwe juu yake na baba yake-: Ya kwamba mwanamke mmoja alipatikana akiwa kauwawa katika moja ya vita vya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akakemea vikali Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuuwawa wanawake na watoto.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliona mwanamke akiwa kauwawa katika moja ya vita, akakemea vikali kuuwawa wanawake na watoto ambao hawajafikia balehe.

Mafunzo
  1. Mwanamke na mtoto yeyote ambaye hatopigana, na mwenyekuwa mfano wao kama wazee vikongwe, na watawa, hawa hawauawi, madam hawajatoa rai au msaada wowote wa kuwapiga waislamu, ikiwa watafanya hivyo basi nao watauawa.
  2. Katazo la kuwaua wanawake na watoto; kwa sababu hawa huwa hawawapigi vita waislamu, na malengo ya kupigana katika njia ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, ni kuvunja nguvu ya wapiganaji pekee, ili ujumbe wa haki uwafikie watu wote.
  3. Huruma ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake mpaka katika mapambano na vita.
Marejeo

صحيح البخاري (4/ 61) (3014). صحيح مسلم (3/ 1364) (1744). الإلمام بشرح عمدة الأحكام، لإسماعيل الأنصاري (2/ 189). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، للبسام (ص746).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Adabu za Jihadi.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com

Ya kwamba mwanamke mmoja alipatikana akiwa kauwawa katika moja ya vita vya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akakemea vikali Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuuwawa wanawake na watoto · Hadithi zenye maelezo · Sabīl