Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Ubora na Fadhila za Funga.

Hadithi 5

Amesema Mwenyezi Mungu: Kila amali ya mwanadamu hiyo ni ya kwake isipokuwa swaumu, bila shaka hiyo ni yangu na mimi ndiye ninayeilipa

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «قَالَ اللَّهُ: كُلُّ عَمَلِ ابْنِ آدَمَ لَهُ، إِلَّا الصِّيَامَ، فَإِنَّهُ لِي وَأَنَا أَجْزِي بِهِ، وَالصِّيَامُ جُنَّةٌ، وَإِذَا كَانَ يَوْمُ صَوْمِ أَحَدِكُمْ فَلاَ يَرْفُثْ وَلاَ يَصْخَبْ، فَإِنْ سَابَّهُ أَحَدٌ أَوْ قَاتَلَهُ، فَلْيَقُلْ إِنِّي امْرُؤٌ صَائِمٌ، وَالَّذِي نَفْسُ مُحَمَّدٍ بِيَدِهِ، لَخُلُوفُ فَمِ الصَّائِمِ أَطْيَبُ عِنْدَ اللَّهِ مِنْ رِيحِ المِسْكِ، لِلصَّائِمِ فَرْحَتَانِ يَفْرَحُهُمَا: إِذَا أَفْطَرَ فَرِحَ، وَإِذَا لَقِيَ رَبَّهُ فَرِحَ بِصَوْمِهِ».
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Amesema Mwenyezi Mungu: Kila amali ya mwanadamu hiyo ni ya kwake isipokuwa swaumu, bila shaka hiyo ni yangu na mimi ndiye ninayeilipa, na swaumu ni kinga, na itakapokuwa ni siku ya kufunga mmoja wenu basi asitamke machafu, wala asifanye fujo, na ikiwa kuna mtu atamtukana au akampiga, basi aseme, mimi nimefunga, namuapa yule ambaye nafsi ya Muhammadi iko mkononi mwake, hakika harufu ya mdomo wa mfungaji ni nzuri mno mbele ya Mwenyezi Mungu kuliko harufu ya Miski, mfungaji anafuraha mbili anazofurahia: Anapofuturu hufurahi, na akikutana na Mola wake atafurahi kwa swaumu yake"
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema katika hadithil Kudsi kuwa: Amali zote za mwanadam mema huzidishwa jema moja kwa mara kumi mfano wake mpaka ziada mia saba, isipokuwa swaumu; kwani hiyo ni yangu kiasi kwamba huwa haifikiwi na ria, na mimi ndiye ninayeilipa, hivyo ninabaki peke yangu katika kujua kiwango cha thawabu zake na uzidishwaji wa mema yake. Kisha akasema: "Na swaumu ni kinga" Ni kinga na ni ngome madhubuti dhidi ya moto; kwa sababu ni kujizuia na matamanio na kutumbukia katika madhambi, na moto umezingirwa na matamanio. "Itakapokuwa ni siku ya kufunga kwa mmoja wenu basi asifanye machafu" kwa tendo la ndoa na vitangulizi vyake, wala kwa maneno machafu moja kwa moja. "Wala asifanye fujo" Kwa ugomvi na zogo. "Na ikiwa mtu atamtukana au kumpiga" Katika mwezi wa Ramadhani basi na aseme: Mimi ni mtu niliyefunga; huenda akamuacha, ikiwa ataendelea na kukawa hakuna namna zaidi ya kupigana naye pasina utani basi na amsukume kidogo kidogo kama anamtenza nguvu. Kisha akaapa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na akamuapia yule ambaye nafsi yake iko mkononi mwake kuwa kubadilika kwa harufu ya kinywa cha mfungaji kwa sababu ya swaumu hiyo ni nzuri mno mbele ya Mwenyezi Mungu siku ya Kiyama kuliko harufu ya Misiki kwenu, na inamalipo mengi kuliko Miski iliyohimizwa katika swala za Ijumaa na vikao vya kumtaja Mwenyezi Mungu. Na mfungaji anafuraha mbili anazofurahia: Anapofungua anafurahia kufungua kwake kwa kuondoka njaa yake na kiu yake kwa kuhalalishiwa kufungua, na anafurahi kwa kutimia swaumu yake na kufikia kikomo kwa ibada yake, na wepesi kutoka kwa Mola wake Mlezi, na nimsaada kwa mustakabali wa swaumu yake. "Na akikutana na Mola wake Mlezi atafurahi kwa swaumu yake" Kwa malipo yake na thawabu zake.

Mafunzo
  1. Fadhila za swaumu nakuwa inamuhifadhi mfungaji katika dunia kutokana na matamanio, na Akhera kutokana na adhabu ya Moto.
  2. Miongoni mwa adabu za swaumu ni kuacha maneno mabaya na ya hovyo, na kusubiri dhidi ya maudhi ya watu na kukabiliana na maudhi hayo kwa subira na ihisani.
  3. Swaumu au mwenye kumuabudu Mwenyezi Mungu anapofurahi kwa sababu ya kukamilisha ibada yake na kuimaliza hilo halipunguzi malipo yake Akhera.
  4. Furaha kamili inakuwa kwa kukutana na Mwenyezi Mungu Mtukufu, pale wanapotimiziwa wenye subira na wafungaji malipo yao pasina hesabu.
  5. Kuwafahamisha watu kwa ibada uliyonayo wakati wa haja na masilahi si katika riyaa kwa kauli yake: "Hakika mimi nimefunga".
  6. Mfungaji iliyekamilika swaumu yake ni yule viliyefunga viungo vyake kutokana na madhambi, na ulimi wake kutokana na uongo na machafu, na kusema uongo, na tumbo lake kutokana na chakula na vinywaji.
  7. Katazo la kufanya fujo na ugomvi na zogo wakati wa swaumu limetiwa mkazo, lakini pia yamekatazwa hayo kwa mtu asiyekuwa katika swaumu.
  8. Hadithi hii ni katika yale anayoyapokea Mtume rehema na amani ziwe juu yake kutoka kwa Mola wake Mlezi, na huitwa Hadithi ya kiuungu, nayo ni ile ambayo matamshi yake na maana yake imetoka kwa Mwenyezi Mungu, isipokuwa haina mambo maalumu kama ya Qur'ani ambayo inatofautiana kwayo na maneno mengine, ikiwemo kukitumia kisomo chake kama ibada na kuwa twahara (msafi) na kutoa changamoto na maswala kisayansi na mengineyo.
Marejeo

صحيح البخاري (3/ 26) (1904). صحيح مسلم (2/ 807) (1151). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 357). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (2/ 866). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (15/ 5). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (5/ 265).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Hakika Peponi kuna mlango unaoitwa Rayyani, watauingia wafungaji siku ya Kiyama, hato ingia ndani ya Pepo hiyo isipokuwa wafungaji

عَنْ ‌سَهْلٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «إِنَّ فِي الْجَنَّةِ بَابًا يُقَالُ لَهُ الرَّيَّانُ، يَدْخُلُ مِنْهُ الصَّائِمُونَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ، لَا يَدْخُلُ مِنْهُ أَحَدٌ غَيْرُهُمْ، يُقَالُ: أَيْنَ الصَّائِمُونَ، فَيَقُومُونَ لَا يَدْخُلُ مِنْهُ أَحَدٌ غَيْرُهُمْ، فَإِذَا دَخَلُوا أُغْلِقَ، فَلَمْ يَدْخُلْ مِنْهُ أَحَدٌ».
Imesimuliwa kutoka kwa Sahal Mwenyezi Mungu amridhie, kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Hakika Peponi kuna mlango unaoitwa Rayyani, watauingia wafungaji siku ya Kiyama, hato ingia ndani ya Pepo hiyo isipokuwa wafungaji, kutasemwa: Wapo wapi wafungaji? Watasimama hatoingia ndani yake isipokuwa wao, watakapoingia utafungwa kisha hatoingia ndani yake yeyote".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba mlango mmoja miongoni mwa milango ya Pepo unaitwa: Mlango wa Rayyan, wataingia hapo wafungaji siku ya Kiyama, hatoingia yeyote zaidi yao, patanadiwa: Wako wapi wafungaji, basi watasimama na wataingia, hatoingia hapo yeyote zaidi yao, atakapomaliza kuingia wa mwisho wao utafungwa, na hatoingia tena yeyote.

Mafunzo
  1. Amesema Nawawi: Katika hadithi hii kuna ubora wa swaumu na heshima kwa wafungaji.
  2. Mwenyezi Mungu amewatengea wafungaji mlango katika milango minane ya Pepo, watakapouingia utafungwa.
  3. Kumebainishwa kuwa Pepo inamilango.
  4. Amesema Assanadi: Kauli yake: "Wako wapi wafungaji", yaani: Wenye kukithirisha kufunga, kama mtu muadilifu na dhalimu, husemwa kwa mtu aliyezoea hilo, na si kwa mwenye kufanya hilo mara moja.
  5. "Rayyan" Yaani: Mwenye kukata kiu; kwa sababu wafungaji hupata kiu na hasa hasa katika siku za kiangazi zenye joto la muda mrefu; watalipwa kwa kuitwa mlango huu kwa kile kilichokuwa kinawahusu wao, mlango wa Rayyan, na imesemekana kuwa Rayyan ni wingi wa kulowesha koo kinyume cha kiu, na umeitwa hivyo; kwa sababu ndio malipo ya wafungaji kwa kiu yao na njaa yao.
Marejeo

صحيح البخاري (3/ 25) (1896). صحيح مسلم (2/ 808) (1152). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 360). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (2/ 868). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (5/ 270).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Atakayefunga Ramadhani kwa imani na kutaraji malipo toka kwa Allah, atasamehewa madhambi yake yaliyotangulia

عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «مَنْ صَامَ رَمَضَانَ إِيمَانًا وَاحْتِسَابًا غُفِرَ لَهُ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبِهِ»
Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakayefunga Ramadhani kwa imani na kutaraji malipo toka kwa Allah, atasamehewa madhambi yake yaliyotangulia"
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayefunga mwezi wa Ramadhani kwa kumuamini Mwenyezi Mungu, na kwa kuitakidi ulazima wa swaumu na yale aliyoyaahidi Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa wafungaji kuwa na malipo makubwa na thawabu, akikusudia kupata radhi za Allah Mtukufu si kwa kutaka kujionyesha au kusikika, yatasamehewa kwake madhambi yake yaliyopita.

Mafunzo
  1. Fadhila za kutakasa matendo, na umuhimu wake katika funga ya Ramadhani na amali njema nyinginezo.
Marejeo

صحيح البخاري (1/ 16) (38). صحيح مسلم (1/ 523) (760). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 361). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمصطفى الخِن وغيره (2/ 868). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (15/ 40). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (5/ 270).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Enyi kongamano la vijana mwenye uwezo miongoni mwenu wa kuoa na aoe, kwani ndoa ni sababu ya kuinamisha macho na kulinda tupu, na asiekuwa na uwezo basi ajilazimishe kufunga, hakika funga kwake itakata matamanio

عَن عَبْدِ اللَّهِ بنِ مَسْعُودٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: كُنَّا مَعَ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَ: «مَنِ اسْتَطَاعَ البَاءَةَ فَلْيَتَزَوَّجْ، فَإِنَّهُ أَغَضُّ لِلْبَصَرِ، وَأَحْصَنُ لِلْفَرْجِ، وَمَنْ لَمْ يَسْتَطِعْ فَعَلَيْهِ بِالصَّوْمِ، فَإِنَّهُ لَهُ وِجَاءٌ».
Kutoka kwa Abdallah bin Masudi radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Siku moja tulikuwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema: "Enyi kongamano la vijana mwenye uwezo miongoni mwenu wa kuoa na aoe, kwani ndoa ni sababu ya kuinamisha macho na kulinda tupu, na asiekuwa na uwezo basi ajilazimishe kufunga, hakika funga kwake itakata matamanio".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Mtume rehema na amani ziwe juu yake amewahimiza wenye uwezo wa tendo la ndoa na gharama ya ndoa waoe; kwani hilo Iinahifadhi macho yake kutokana na mambo yaliyokatazwa, linalinda usafi wake wa mwili, na linamzuia asiingie katika uasherati, ambaye hawezi kukidhi mahitaji ya ndoa hali ya kuwa ana uwezo wa kufanya tendo la ndoa basi ni lazima afunge, kwani hii itakata matamanio ya tupu na shari ya manii.

Mafunzo
  1. Uislamu umechunga sana sababu za mtu kujizuia na machafu na kusalimika na machafu.
  2. Himizo la kufunga swaum kwa ambaye hatoweza gharama za ndoa; kwa sababu hudhoofisha matamanio.
  3. Kufunga kunafananishwa na kuhasiwa; Kwa sababu kuhasi ni kuchubua mishipa ya korodani mbili, na kwa kitendo hicho hupotea matamani ya tendo la ndoa, hivyo hivyo swaumu hudhoofisha hamu ya tendo la ndoa.
Marejeo

صحيح البخاري (3/ 26) (1905). صحيح مسلم (2/ 1018) (1400). الإلمام بشرح عمدة الأحكام للشيخ ،لإسماعيل الأنصاري (2/ 57). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، لعبد الله البسام (ص565). خلاصة الكلام شرح عمدة الأحكام، لفيصل آل مبارك (ص281).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Inapokuja Ramadhani hufunguliwa milango ya pepo na hufungwa milango ya moto, na mashetani hufungwa minyororo

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ أَنَّ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: «إِذَا جَاءَ رَمَضَانُ فُتِّحَتْ أَبْوَابُ الْجَنَّةِ، وَغُلِّقَتْ أَبْوَابُ النَّارِ، وَصُفِّدَتِ الشَّيَاطِينُ».
Kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Inapokuja Ramadhani hufunguliwa milango ya pepo na hufungwa milango ya moto, na mashetani hufungwa minyororo".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa unapoingia mwezi wa Ramadhani hutokea mambo matatu: La kwanza: Hufunguliwa milango ya pepo na haufungwi mlango wowote katika milango hiyo. La pili: Hufungwa milango ya moto na haufunguliwi mlango wowote katika hiyo. La tatu: Hufungwa minyororo mashetani na majini wakaidi, hawaachwi kuendelea na yale waliyokuwa nayo katika miezi mingine isiyokuwa Ramadhani. Na yote hiyo ni kwa kuutukuza mwezi wa Ramadhani, na kumhamasisha mtendaji kukithirisha ibada, kama swala na sadaka, na dhikiri na kusoma Qur'ani na mengineyo; na kujitenga mbali na madhambi na maasi.

Mafunzo
  1. Fadhila za mwezi wa Ramadhani.
  2. Habari njema kwa wafungaji ndani yake kuwa mwezi huu mtukufu ni msimu wa ibada na kheri.
  3. Katika kufungwa mashetani ndani ya Ramadhani ni ishara ya kuondolewa udhuru kwa kila aliyelazimishwa kutekeleza sheria na ni kana kwamba anamwambia:
  4. Amesema Al-Qurtubi: Ikiwa patasemwa: Inakuwaje tunaona shari na maasi yanatokea ndani ya Ramadhani kwa wingi, na kama mashetani yangefungwa basi tusingeona? Jawabu: Ni kuwa maasi hupungua kwa wafungaji swaumu ambayo zimehifadhiwa sharti zake na zikazingatiwa adabu zake, au nikuwa wanaofungwa ni baadhi ya mashetani nao ni wale wakaidi na si wote kama ilivyotangulia katika baadhi ya riwaya, au makusudio yake ni kupungua kwa shari ndani yake, na jambo hili linaonekana, kwani kutokea kwake ni mara chache kuliko miezi mingine, kwani si lazima kufungwa wote kuwa kusitokee shari wala maasi; kwa sababu hilo lina sababu zingine zisizokuwa mashetani kama nafsi chafu na mazoea mabaya na mashetani wa kibinadamu.
Marejeo

صحيح البخاري (3/ 25) (1899). صحيح مسلم (2/ 758) (1079). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 362). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (5/ 273). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (15/ 46). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 869).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com